HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 22, 2023

GFP International Kijenga Karakana ya Kimaifa ya Uchomeleaji

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Shirika la GFP International kujenga karakana ya umahiri ya Uchomeleaji  Chuo cha Ufundi Don Bosco Jijini Dar es Salaam.

Kujengwa Karakana hiyo itakuwa ndio Karakana ya kwanza kwa Afrika Mashariki  ambapo vyeti vikitolewa katika chuo hicho vitambulika Kimataifa.

Akizungumza wakati sherehe za kujengwa Karakana hiyo katika Chuo cha Don Bosco  Mwasisi wa GFP International  Michael Vallez amesema kuwa ujenzi wa huo utazingatia viwango vya kimataifa na walimu ambao watakwenda kusoma umahiri nchini Afrika Kusini ndio watakuwa Walimu katika Karakana hiyo ya Kisasa.

Amesema kuwa fani ya uchomeleaji iko katika sekta nyeti za mafuta na Gesi ambapo wanaofanya kazi hiyo lazima wawe na vyeti vya Kimataifa vya kuweza kuomba kandarasi kwenye sekta hiyo.

Vallez amesema kuwa umahiri katika uchomeleaji ndio unahitajika kwani kampuni nyingi zinahitaji kuwa na wakandarasi wenye viwango vya kimataifa.

Mkurugenzi Mkazi wa GFP International  Hilu Bura amesema kuwa dunia imebadilika wenye ujuzi na ufundi  wanahitaji  kuendeleza katika viwango vya kimataifa.

Bura amesema kuwa Tanzania tumebarikiwa kujengewa chuo cha umahiri hivyo kitapoanza chuo watu wasome na wasiposoma watakuja watu kutoka nchi nyingine watasoma na miradi mikubwa watakuwa wao ndio wenye sifa za kufanya.

Bura amesema ni bahati kupata watu wa kuwasomesha nje ya nchi hivyo wanaokwenda wakazingatie ili kuleta tija kwenye Taifa.
Mwalimu wa Uchomeleaji wa Don Bosco Erick Nkula amesema kuwa wanategemea kuzalisha watu wengi na nje ya nchi.

Amesema Don Bosco kujengwa kwa Chuo hicho watakuwa wametimiza ndoto watakwenda mbali huku mahitaji yataongezeka katika udahili.

Amesema kuwa katika ujenzi wa karakana ya umahiri utaendana na vifaa ambavyo vinatambulika kimataifa na hata ujenzi wa jengo ni kutambulika Kimataifa.

Picha ya pamoja kati ya GFP International na Don Bosco mara baada ya kuhitimisha juu ya kuanza kwa ujenzi wa karakana ya kisasa.
Mwalimu wa Uchomeleaji wa Chuo cha Don Bosco  Erick Nkula akizungumza faida ya ujenzi wa karakana ya kisasa ya uchomeleaji katika chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mwasisi wa GFP International Michael Vallez  akiwa na baadhi ya watendaji wa GFP wakiwa na majembe kuashiria sehemu itakayojengwa Karakana ya Umahiri ya Uchomeleaji Don Bosco, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkazi GFP International Hilu Bura akizungumza kuhusina juu ya faida ya umahiri wa kutambulika kimataifa katika Uchomeleaji , jijini Dar es Salaam.
Mwasisi wa GFP International Michael Vallez akizungumza katika Chuo cha Don Bisco kuhusiana Ujenzi wa Karakana ya Kisasa ya Kisasa ya Uchomeleaji itakayotambulika Kimataifa,  jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad