HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 5, 2023

BODA BODA WALIA NA UHABA WA PETROLI

WATUMIAJI wa usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda katika mamlaka ya mji mdogo wa Katoro mkoani Geita wameililia serikali juu ya uhaba wa mafuta ya petroli unaoendelea mkoani humo ambapo kwa siku ya leo mafuta yalikuwa yanapatikana katika kituo kimoja tu cha Lake oil kilichopo Nyamigota huku vingine vikiwa vimefungwa .

Wakizungumza na Michuzi Tv bodaboda hao waliwashutumu wamiliki wa vituo vya mafuta kuficha mafuta na kugoma kuyauza huku wakisubiri tamko kutoka kwa serikali la kupandisha mafuta ili wapate faida zaidi.

Kwa Upande wa meneja wa sheli ya Faraja Juma Adam alisema mafuta yamekuwa ya tabu kupatikana hata kwa upande wao pia kwani wanapata mafuta machache kulingana na matumizi ya mjini hapo.

Aidha wananchi hao walisema kuwa ukosefu wa mafuta umekuwa ni kilio kikubwa kwao kwani wengi wao wanaishi kwa kutegemea biashara za kubeba watu kwenye bodaboda yanapoadimika kama hivi inakuwa ngumu sana kwao kuendesha maisha.


Waendesha Pikipiki Maarufu kama Boda boda wa Katoro mkoani Geita wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kuweka mafuta ya Petroli.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad