WIMBO WA ENJOY THAT WAZINDULIWA, AKON, BROUWN KUSHIRIKIANA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 11, 2023

WIMBO WA ENJOY THAT WAZINDULIWA, AKON, BROUWN KUSHIRIKIANA

 

MWIMBAJI wa  Muziki Nchini Marekani- Multtalent Akon ameunagana na mkali wa Afrika Kusini Brown wanatarajia kuachia wimbo wao uitwao  'Enjoy That' hivi karibuni.

Wimbo huu wa kusisimua, utazinduliwa chini ya lebo ya Muziki ya Akon maarufu ya Konvict Kulture na ngoma hii ni msingi wa kuvutia wa EP ijayo inayosubiriwa kwa hamu ya 'Afro Freak' ambayo itakuwa na sauti za kuvutia, midundo isiyozuilika kusikilizika na midundo ya kusisimua inayoongozwa na amapiano "Enjoy That"ambayo ipo tayari kutawala chati za muziki ulimwenguni.

"Kufanya kazi na  mwanamuziki Brown ilikuwa safari ambayo ilituwezesha kuunda kitu cha pekee kwenye ngoma yetu ya 'Enjoy That'. Amesema Akon katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni.

 Inajumuisha kiini cha kuishi bila majuto, kuthamini burudani za maisha na kufurahia kila toleo linalotolewa kwa utayarishaji wake mahiri na maneno ya kutia moyo katika wimbo huo unaangazia hali za watu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad