HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 17, 2023

Wadau wa Usafirishaji kwa njia ya Maji waipongeza TASAC

Mkurugenzi wa Udhibiti kwa njia ya Maji wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC ) Deogratius Mukasa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa wadau wa Usafirishaji kwa njia ya Maji uliofanyika jijini Dar es Salaam.


 *Ni katika kupata elimu ya kanuni katika sekta hiyo

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
WADAU wa sekta ya usafiri kwa njia ya maji wamesema kuwa wakati wa sasa ni kufanya kazi kutokana na serikali kupitia Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kuwashirikisha masuala mbalimbali ambayo yanafanya sekta hiyo kuimarika.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa wadau wa usafirishaji kwa njia ya Maji Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) Edward Urio amesema kuwa TASAC imesikia kilio chao cha kanuni mbalimbali ambazo zimekuwa ni kikwazo katika utendaji wao wa kila siku hivyo baada ya kukutana wamejadiliana na kufikia mahala pazuri kuinyesha njia ya kuendelea kuimarika kwa biashara.

Urio amesema maboresho yaliyofanyika yamegusa maeneo yaliyokuwa na utata mwingi katika utendaji wao na kusema serikali ya awamu ya sita imesimamia masula ya msingi kwa wadau wa Forodha

Amesema upande wa mawakala wa forodha walikuwa na utata katika ule muda wa kontena linaposhuka bandarini na linapofika kwenye bandari kavu ambako kulikuwa na upotevu wa siku mbili au tatu kwa kuhoji jambo hilo lilipaswa kubebwa na nani jambo ambalo kanuni hizo zimekuja na majibu yake na kutua mzigo wa kwa mawaka la hao.

Urio amesema kuna suala la uagizaji mzigo kwa kupitia bandari hasa mzigo wa makasha, kuna utaratibu ambao unatakiwa uweke dhamana ya kuweza kuaminiwa na wale mawakala wa meli uweze kulichukua lile kasha ukapakue mzigo wako ambapo wakala alitakiwa kulipa dhamana ya kasha kwa kuweka dola za kimarekani 3000 hadi 500 mpaka litaporudi hali iliyofanya kuwa ni mzigo ambapo baadhi ya wafanyabiashara kushindwa dhamana hiyo.

“Kama ni hapa Dar es Salaam, kama ni Morogoro, kama ni Arusha, kama ni Malawi, Zambia, Kongo, halafu ile dhamana ya lile kontena inakuwa iko chini kwa wakala wa forodha mpaka litakapokuwa limerudi kwenye sehemu yake husika ya kurudisha kwa mawakala wa bima kuchukua dhamana ya makasha hayo ,” amesema.

“Tulikuwa tunatakiwa kuweka takribani dola 3000 mpaka 5000 kwenye makasha ya futi 40 na dola 1000 mpaka 2000 kwenye makasha ya futi 20. Unakuta kuwa ukiwa na kontena 10 ya futi 40 unatakiwa ulipe takriban dola elfu 40,” amesema.

Amesema dola hizo 40000kwa wakala ambaye analipwa dola 200 kwa kila kontena ilikuwa ni maumivu makubwa.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Meli Tanzania Esther Mbuya amesema kuwa Mkutano kati ya TASAC na Wadau wa usafirishaji kwa njia ya maji nj mkutano wenye kuleta afya ya utendaji.

Amesema kutokana elimu walioipata watakwenda kuelimisha wadau namna ya kuboresha zaidi pasipo kuleta tofauti baina ya taasisi ya udhibiti.

Mkurugenzi wa Udhibiti Huduma za Usafiri kwa njia ya maji TASAC, Deogratias Mukasa amesema wamekutana na wadau wao kutoa ufafanuzi kuhusu kanuni mpya nne ambazo zimepitishwa Juni mwaka huu na Waziri mwenye dhamana ya Ujenzi na Uchukuzi.

Amesema kanuni hizo zinahusu usalama wa mizigo, utendaji wa shughuli ndani ya bandari na bandari kavu, usajli wa wasafirishaji wanaouza na kusafirisha bidhaa kutoka Tanzania kwenda nchi za nje kupitia bandari, pamoja na ya uhakiki shehena na ya uwakala wa meli.

Wadau waliokutana nao ni bandari, bandari kavu, mawakala wa meli, wagomboaji wa shehena, wakusanyaji na watawanyaji shehena, wasafirishaji na mamlaka ya forodha.

Amesema shirika hilo linathamini utoaji elimu kabla ya kuanza utekelezaji wa sheria au kanuni zake, na kwamba maboreesho ya kanuni hizo yanalenga kuboresha utoaji huduma kwa usahihi na kuleta usawa kwa wadau wote.
Mkurugenzi wa Udhibiti kwa njia ya Maji wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC ) Deogratius Mukasa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa wadau wa Usafirishaji kwa njia ya Maji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Meli Tanzania Esther Mbuya akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa usafirishaji kwa njia  maji uliofanyika jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad