VIFO NJE NJE NGORONGORO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 23, 2023

VIFO NJE NJE NGORONGORO

 


-Wanyama wakali wazidi kumaliza watu
-Mchungaji kijana ajeruhiwa vibaya na nyati akichunga asubuhi kweupe
-Majeruhi asota porini saa kibao kutokana na ukosefu wa mawasiliano
-Ni mtiririko luluki wa vifo vya nguvu kazi kuuliwa na wanyama wakali.
-Vijana wenzake waomba Serikali iwahamishe haraka

Na Mwandishi wetu
SIKU chache baada ya kuripotiwa kwa majeruhi aliyepoteza viganja na sehemu kubwa ya uso wake kutokana na Kuvamiwa na fisi kwa mkazi wa Sapai kijijini Irkepusi wilayani Ngorongoro Rose Kapande,

Taarifa za watu kujeruhiwa na wanyama wakali katika eneo hilo zimezidi kuripotiwa huku tukiarifiwa kila siku matukio hao hurekodiwa kwa namna tofauti tofauti

Miongoni mwa matukio maarufu wilayani humo ni pamoja na watoto kuliwa na Simba, wanawake Kuvamiwa na chui, mifugo kuliwa na wanyama wakali nakadharika jambo linaloashiria kukosekana Kwa usalama wa uhakika Kwa wananchi wa eneo hilo

Taarifa zilizoshuhudiwa na gazeti hili zinasema kuwa juzi tarehe 21 Agosti muda wa saa tatu asubuhi mwananchi mmoja akiwa machungani alijeruhiwa vibaya na MBOGO maeneo LOLTUROTO- Loomunyi.

Taarifa zinasema kuwa eneo hilo alipojeruhiwa hapakuwa na mawasiliano kabisa!
Mmoja wa majeruhi aliyejeruhiwa na mbogo huyo akiwa machungani ni NIAYOK KOLONJO TUYAI.

mkazi wa meshili mwenye umri wa miaka 30, kabila la kimasai ambaye alijeruhiwa vibaya maeneo ya shingoni na usoni jambo lililopelekea kutokwa na damu nyingi

Taarifa zinaongeza kuwa kutokana na majeruhi kutokuwa na simu na eneo alilopata ajali hiyo kutokuwa na mawasiliano ilimchukua saa kadhaa akiteseka bila kupata msaada hadi timu ya waangalizi wa wanyama walipopita na kumuokota na hatimaye kumkimbiza hospitali ya Fame iliyopo Karatu mjini.

Wakizungumza Kwa nyakati tofauti wananchi wa maeneo hayo wameiomba Serikali kuongeza kasi katika kuwahamisha wananchi kwani hali yao ni mbaya kutokana na mtiririko wa matukio lukuki

"Serikali ituhamishe haraka, Leo umesikia hili la kujeruhiwa na nyumbu, lakini juzi mlirupoti aliyeliwa na Fisi, wapo watoto juzi kati hapa waliliwa na Simba wakitoka malishoni, kwa kifupi ni hatari sana". Alisema Tengesi Ole Shangai mkazi wa Ngorongoro

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad