TCAA yahamasisha matumizi ya Drones - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 4, 2023

TCAA yahamasisha matumizi ya Drones

 


*Kutumia katika umwagiliaji na unyunyuziaji dawa

Na Chalila Kibuda Michuzi TV
MAMLAKA ya Anga Tanzania (TCAA) imesema kuwa katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane imejipanga kutoa elimu ya matumizi ya ndege isiyo na Rubani 'Drones' katika kutumia kwenye kilimo kwa matumizi ya umwagiliaji na unyunyuziaji wa dawa.

Hayo ameyasema Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa TCAA Yassaya Mwakifulefule kwenye Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale , jijini Mbeya.

Amesema kuwa ndege hiyo inaweza kutumika kumwagilia maji kwa kuanzia hekari 25 ambapo inamrahisishia mkulima kutumia muda mdogo kuliko kwa kutumaia mpira.

Amesema kuwa Teknolojia imerahisisha wakulima kuweza kutumia nguvu ndogo kuliko kutumia mbinu za kizamani.

Mwakifulefule amesema kuwa ni fursa kwa sekta ya kilimo kwa wakulima kuweza kutumia teknolojia hiyo kwa kununua na kujisajili pamoja na kupata mafunzo ya namna ya kutumia Drones.

Amesema kuwepo kwa mafunzo na kujisajili inatokana na kuweka usalama wa anga kwani ndege hiyo ikiruka kwenye anga ya ndege ya abiria madhara yake ni makubwa.

Aidha amesema kuwa mafunzo ya matumizi ya ndege hiyo ni wiki nne ambapo atatunukiwa cheti cha utambuzi wa kwenda kurusha ndege isiyo na rubani kwenye shughuli mbalimbali.

Amesema kuwa watu wanaomiliki Drones na kuzitumia bila kujisajili na bila mafunzo ni kosa la kisheria hivyo wanatakiwa kufuata sheria hiyo.

Mwakifulefule amesema kuwa katika kutoa huduma ya usafiri wa anga ni kutaka kuwa na usalama kwa ajili ya ndege zinazopita katika anga ya Tanzania.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad