TASAC yawataka wananchi kutembelea banda Maonesho ya Nane Nane Mbeya - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 2, 2023

TASAC yawataka wananchi kutembelea banda Maonesho ya Nane Nane Mbeya

Mwananchi akisaini kitabu na kutoa maoni yake juu ya majukumu ya TASAC wakati alipotembelea banda la TASAC Maonesho ya Kimataofa ya Kilimo kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA  la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ni kati ya Taasisi za Kiserikali zinazoshiriki Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima yanayotambulika kama NaneNane kwa ajili ya kutoa elimu ya majukumu ya shirika hilo.

Maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya NaneNane Mkoani Mbeya yameanza tarehe 1 Agosti na kilele chake ni tarehe 8 Agosti, 2023.Kauli mbiu ya maonesho hayo ni:- “Tanzania: Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo ya Chakula na Usalama wa Chakula ”.

TASAC inashiriki maonesho hayo ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi na majukumu yanayotekelezwa na TASAC kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415.

Katika moja ya majukumu ya TASAC ni usalama wa vyombo vya usafiri majini ikiwemo, mitumbwi na meli ndogo za uvuvi ambayo ni moja kwa moja wanagusa wananchi kwenye sekta ya uvuvi kutoa elimu.

TASAC inawaalika wananchi wote kutembelea banda la TASAC lipo katika eneo zilipo Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi.
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Calvin akizungumza na wananchi mbalimbali hawapo pichani waliotembelea katika  banda la TASAC kwenye maonesho Kimataifa  ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John
Mwakangale jijini Mbeya.
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Calvin akizungumza na wananchi mbalimbali hawapo pichani waliotembelea katika  banda la TASAC kwenye maonesho Kimataifa  ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John
Mwakangale jijini Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad