MRADI wa kudhibiti Sumukuvu nchini (TANIPAC) inatarajia kujenga maabala ya Rufaa ya kilimo ikiwa ni pamoja na Kuwekea Vifaa.
Akizungumza katika Maonesho ya Nane nane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Mratibu wa Mradi wa TANIPAC, Clepine Josephat amesema kuwa Maabara hiyo itajengwa katika mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma na itakuwa ya ghorofa tano kwaajili ya kukabiliana na tatizo hilo.
Amesema kuwa hapo awali Sampo za Mazao yenye sumu Kuvu yalipelekwa nchini Marekani na Ujerumani lakini kwa sasa watejenga maabala hiyo hapa nchini.
"Sampo zote sasa zitapimwa hapa nchini kwaajili ya kuhakikisha mazao yote yanakidhi Vigezo katika mazao yote yanayozalishwa kwenye halmashauri hapa nchini kwaajili ya kukidhi mahitaji ya soko la Mtanana." Amesema
Amesema Mradi huo pia utajenga soko au kituo Mahili za mazao baada ya kuvuna katika eneo la Mtanana pia katika eneo hilo kutakuwa na kiwanda na Chuo cha mafunzo.
Kujenga kituo hicho kwaajili ya lengo la kuunganisha kiwanda na maghara yaliyopo hapa nchini.
Katika hatua nyingine amesema kuwa watajenga maghala (14) ambayo yatatumika kuhifadhia mahindi kwa lengo la kuondoa tatizo la sumukuvu kwenye mazao ya nafaka na mafuta pamoja na kuunganisha na kituo cha Mtanana.
Amesema baada ya ujenzi huo wanunuzi watanunua mazao katika soko hilo badala ya kwenda kununua mazao kwa mkulima.
Sumukuvu inaathiri zaidi mazao ya mahindi na karanga kutokana na namna ya na wakati wa kuvuna na kuhifadhi ambapo unyevuunyevu unaopatikana kwenye mazao husababisha uotaji wa fangasi na kuwa chanzo cha sumukuvu.
Mradi wa TANIPAC unalenga utakapo kamilika kuwezesha jamii kutumia njia sahihi na za kisasa za uhifadhi wa nafaka hususani mahindi kutokana na sumukuvu.
“Tatizo la sumukuvu linasababisha mazao ya wakulima kukosa bei nzuri kwenye masoko, hii hupelekea mkulima kupata hasara” Amesema.

Vihenge vya chuma ambavyo vlitegenezwa kwaajili ya kuwekea mazao ili yasiathiliwe na Sumu Kuvu.
Mmoja wa wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo kupitia Mradi wa TANPAC akionesha kihenge cha Chuma cha Kuwekea Mazao ili yasiathirike na Sumu kuvu, ikiwa ni njia moja wapo ya kukabiliana na changamoto hiyo.
No comments:
Post a Comment