SPORTPESA, TIGO WAJA NA ‘MAOKOTO DEILEE’ - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 21, 2023

SPORTPESA, TIGO WAJA NA ‘MAOKOTO DEILEE’

 


Na Mwandishi Wetu, Da es Salaam
Kampuni ya Michezo ya Kubashiri (Sportpesa) imezindua promosheni mpya ya ‘Maokoto Deilee’ kushirikiana sanjari na Mtandao wa Tigo, Kampeni yenye lengo mahsusi kuwazawadia wateja wao fedha kila siku, wiki na simu janja.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Sportpesa, Sabrina Msuya amesema mwisho wa promosheni hiyo mteja atashinda kiasi cha shilingi Milioni 15 (Tsh. 15,000,000/-).

“Wateja wetu wana fursa ya kushinda zawadi ya Tsh. 20,000/- (Elfu ishirini) kila siku, zawadi ya wiki ni Milioni moja (Tsh. 1,000,000/-) na zawadi kubwa ni Shilingi Milioni kumi na tano (Tsh. 15,000,000/-), kila wiki wateja wawili watajinyakulia simu janja,” amesema Sabrina.

Kwa upande wake, Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Tigo, Kenneth Ndulete amewahimiza wateja wa mtandao huo kuchangamkia fursa kupitia promosheni hiyo ambayo wanashirikiana na Sportpesa.

“Wateja wa mtandao wa Tigo wanaweza kupata zawadi hizo kupitia michezo ya kubashiri ya kupitia tovuti ya Sportpesa au kupiga menu (*150*87#) baada ya kufungua akauti hiyo, unaweza kubashiri kupitia Tigopesa,” amesema Ndulete.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad