Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendesha warsha kwa njia ya mtandao kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi ili kuongeza ufanisi kipindi wanapokwenda kufanya mitihani hiyo.
Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno amesema kwa mara ya kwanza wamefanya warsha hiyo kwa njia ya mtandao na kuwakutanisha wanafunzi wa ngazi mbalimbali wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi katika ngazi mbalimbali ikiwa na lengo la kuwanoa kwenye mbinu mbalimbali za mitihani hasa kwenye maeneo yanayokuwa na changamoto kwa watahiniwa wa Bodi.
CPA Maneno amesema yapo Masomo yanaleta changamoto na kiwango cha ufaulu unakuwa mdogo hivyo tumewaletea walimu wa Masomo hayo kutoka vyuo na Taasisi mbalimbali ili waweze kuwapa uzoefu na mbinu mbalimbali za kuweza kujiandaa na kufanya mitihani ya Bodi.
"Tumewasisitiza sana namna ya kujiandaa wasijiandae kiholelaholela bali waweke muda wa kutosha kwenye kujifunza kwani kuna tofauti kubwa sana kati ya watahiniwa wa vyuo na watahiniwa wa mitihani ya Bodi " alisema CPA Maneno
Pia amesema lengo kubwa la NBAA ni kuona wanapandisha kiwango cha ufaulu kwa mitihani mbalimbali pamoja na kuongeza kiwango cha uelewa ili kipindi wanapomaliza mitihani yao waweze kuwa wabobezi kwenye masuala ya Uhasibu na Ukaguzi.
Naye Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo anasema Bodi hiyo imejipanga vizuri ili kuhakikisha kila mtahiniwa anafanya mitihani vizuri na kuhakiksiha wanaondoa changamoto zote.
Meneja wa Huduma za Shirika (NBAA) CPA Kulwa Malendeja akiwakaribisha wakufunzi waliofika kwa ajili ya kutoa mafunzo katika warsha iliyoandaliwa na NBAA kwa njia ya mtandao kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akiwakaribisha wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani mbalimbali ya Bodi ambao walikuwa wakisikiliza Warsha hiyo kwa njia ya mtandao.
Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, CPA Dkt. Emmanuel Christopher akitoa elimu kuhusu namna ya kujiandaa na kufanya masomo ya B1 na C3 kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi waliokuwa wanafuatilia kwa njia mtandao.
Mkufunzi CPA Rashid Mganwa akitoa elimu kuhusu namna ya kujiandaa na kufanya masomo ya B2 na C1 kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi waliokuwa wanafuatilia kwa njia mtandao.
Mkufunzi CPA Nicholas Massawe akitoa elimu kuhusu mabadiliko ya masomo ya Kodi yaani B4 na C4 kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi waliokuwa wanafuatilia kwa njia mtandao mafunzo hayo.
Mkufunzi CPA Ansbert Kishamba akitoa elimu kuhusu namna ya kujiandaa na kufanya somo la B5 kwa wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi.
Well done NBAA. The digital channels and digital modus operandi are the only ways to survive in the future of the profession. Let us keep it up.
ReplyDelete