MISS TANZANIA 2022 KUIWAKILISHA TANZANIA 71st MISS WORLD NCHINI INDIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 18, 2023

MISS TANZANIA 2022 KUIWAKILISHA TANZANIA 71st MISS WORLD NCHINI INDIA

Miss Tanzania 2022 Halima Kopwe kuwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo  ya  dunia  '71st Miss World' yatakayofanyika   Delhi , India tarehe 9 December 2023

Warembo wote akiwemo Halima  watapokelewa tarehe 8 November kwa ajili ya kuanza kambi rasmi ya msahindano kwa muda wa mwezi mmoja  kabla ya fainali

Kama ilivyoutaratibu siku chache kabla ya kuanza safari Miss Tanzania anatarajiwa  kukabidhiwa bendera ya Tanzania ili kuagwa rasmi na Waziri wa Habari Tamaduni Sanaa na Michezo

Mbali na kwenda kushindana Miss Tanzania atatumia fursa hii kutangaza utalii na Taifa la Tanzania katika jukwaa la dunia Watanzania na wadau wote wa sanaa burudani na michezo wakiwemo wanahabari tuungane kumpa nguvu mwakilishi wetu katika mashindano haya makubwa ya dunia.

Kwa habari zaidi na muendelezo wa matukio yanayojiri yatawekwa kwenye ukurasa rasmi wa Miss Tanzania kwenye mitandao ya jamii @misstanzaniaorganisation 



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad