MENEJIMENTI, WAKUU WA VITENGO NACTVET WAFUNDWA MAWASILIANO SERIKALINI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 25, 2023

MENEJIMENTI, WAKUU WA VITENGO NACTVET WAFUNDWA MAWASILIANO SERIKALINI

 NACTVET kupitia kitengo cha Habari na Masoko imeendesha mafunzo juu ya nafasi na umuhimu wa mawasiliano serikalini, 24 Agosti, 2023 Jijini Dar es Salaam.


Mafunzo hayo ambayo ni awamu ya kwanza yamefanyika kwa ajili ya Menejimenti na Wakuu wa vitengo kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao kufanya mawasiliano kwa misingi iliyowekwa kisheria na kikanuni ili kuboresha utoaji na upashanaji taarifa kuanzia ngazi ya taasisi ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi za Kiserikali katika taasisi za umma.

Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dkt. Adolf Rutayuga ambaye pia ameshiriki mafunzo hayo, amewataka washiriki wote kuzingatia na kuheshimu, mifumo ya mawasiliano kwa umma kwa kushirikiana kwa karibu na *kitengo cha habari na masoko cha Baraza.

Dkt.Rutayuga amesema kupitia mafunzo hayo, washiriki katika ngazi zote wamepata mwanga na uelewa mpana juu ya umuhimu wa vitengo vya habari na mawasiliano kwenye taasisi za umma.

Aidha, washiriki walipata fursa ya kupata mafunzo juu ya alama na nembo ya Taifa na matumizi yake katika uchapishwaji wa nyaraka za serikali kulingana na kanuni na miongozo ya nchi.

Wawezeshaji wa mafunzo hayo walikuwa Dkt. Paul Kuhenga kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Bw. George Lugome, Mpigachapa Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.
Katibu Mtendaji wa NACTVET Dkt.Adolf Rutayuga akizungumza katika mkutano wa mafunzo ya Mawasiliano Serikali yaliyoratibiwa na Kitengo cha Habari na Masoko , Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Masoko NACTVET Bw. Jeff Shellembi akitoa maelezo kuhusiana umuhimu wa mawasiliano kwa watendaji namna ya kufanya mawasiliano kwa mifumo iliyowekwa.jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya picha za matukio za washiriki katika mafunzo ya mawasiliano yaliyoratibiwa na Kitengo cha Habari na Masoko NACTVET, Jijini Dar es Salaam.


Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad