MCHAKATO WA MUUNGANO KATI YA TWIGA CEMENT NA TANGA CEMENT WAZIDI KUKUTANA NA VIPINGAMIZI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 21, 2023

MCHAKATO WA MUUNGANO KATI YA TWIGA CEMENT NA TANGA CEMENT WAZIDI KUKUTANA NA VIPINGAMIZI


Na Mwandishi Wetu, Mtaa kwa Mtaa

MCHAKATO wa kuungana wa kampuni mbili za cement za Tanga Cement na Twiga Cement umeendelea kukutana na vikwazo baada ya Jaji anayesimama kama Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani kutoa uamuzi kwa mara nyingine tena muungano huo ni batili na uko kinyume na sheria za nchi.

Kampuni ya Tanga Cement inayomilikiwa kwa asilimia kubwa na kampuni ya Afrisam kutoka Afrika Kusini inayoazimia kuungana na Kampuni maarufu ya Scanscem International DA (Twiga Cement) inayomilikiwa na kampuni mama ya Heilberg group kutoka Ujerumani.

Katika hukumu yake ya pili kuhusiana na suala hilo, Jaji wa Mahakama Kuu, Jaji Fatma Maghimbi ametoa uamuzi kuwa mchakato wa kuziunganisha kampuni hizo tena uliofunguliwa upya na Tume ya Ushindani (FCC) baada ya kubatilishwa na baraza la ushindani ulikuwa kinyume na sheria.

Kwa kuwa baada ya hukumu ya baraza iliyobatilisha muungano huo, Tume ya ushindani haikuwa na mamlaka tena juu ya mchakato huo.

Katika kesi ya rufaa mbele ya Baraza Namba 1 ya mwaka 2023, Kampuni ya kitanzania ijulikanayo kama Chalinze Cement, ilipeleka pingamizi kuhusu mchakato wa muungano kati ya Twiga Cement na Tanga Cement,
ikiambatanisha mapingamizi 11 ya kisheria dhidi ya muungano huo mbele ya Baraza la Ushindani linalokaliwa na Mwenyekiti ambaye ni Jaji wa mahakama kuu na wajumbe wawili wa baraza hilo.

“Maamuzi ya FCC (Tume ya Ushindani) kuruhusu kwa mara ya pili mchakato huo wa muungano kati ya Tanga Cement na Twiga Cement baada ya mchakato wa kwanza wa kuungana kati ya kampuni hizo mbili kubatilishwa na maamuzi ya kimahakama yaliotolewa na baraza la ushindani...

"Yalikuwa ni maamuzi yaliyo kinyume na sheria za nchi, Kampuni hizo mbili zilitakiwa ziombe baraza hili kufanya mrejeo wa maamuzi yake na sio kuanzisha upya mchakato uleule haramu ulioshabatilishwa na maamuzi ya kimahakama ya baraza hili”,amesema Jaji Fatma Maghimbi.

Aidha watoa maamuzi wengine wawili walioketi pamoja na Jaji Maghimbi, kama wajumbe wa baraza la ushindani mbele ya baraza hilo, walitoa uamuzi wa kulitupa nje shauri hilo la rufani kwa sababu mleta shauri hilo kampuni ya Chalinze Cement Company ilifutiwa usaili wake na Brela, hivyo haitambuliki kama kampuni hai kisheria.

Kutokana na kutokuwa hai kwa kampuni hiyo kisheria kunaifanya kampuni hiyo kukosa uhalali wa kisheria kuendesha shauri mahakamani au mbele ya baraza la ushindani.

Jaji Fatma Maghimbi kwa ubobezi wake wa kisheria na kwa kuzingatia maamuzi ya nyuma ya kimahakama, japokuwa alikubali kampuni ya Chalinze Cement Company ilifutiwa usaili wake na Brela hivyo haitambuliki kama kampuni hai kisheria...

Lakini aliona kwa madhumuni ya kuona sheria hazivunjwi na haki ikitendeka alitoa maamuzi kinzani yalio zingatia zaidi mapingimizi ya kisheria yenye tija ambayo tayari yapo mbele ya baraza la ushindani bila kujali yamefikaje.

Hata hivyo kwakuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani, Jaji Maghimbi ameamua kutoa maamuzi kinzani na wajumbe wake, hiyo inaonesha bado kuna vizingiti vikubwa vitavyosababisha ugumu katika ufanikishaji wa mchakato huo wa muungano wa kibiashara.

Pia uamuzi wa Jaji huyo unashabihiana na tamko la Wakili Mkuu wa Serikali aliyekubali usahihi wa mapingamizi matatu yaliyomo kwenye shauri hilo.

Kwakuwa msimamo huu wa Wakili mkuu wa serikali unachukuliwa kama ndio msimamo wa Serikali basi pia ndio msimamo wa Mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ndiye mshauri mkuu wa serikali kwenye masuala yote ya kisheria nchini.

Mchakato huo wa muungano kati ya kampuni hizo mbili, unatakiwa upitiwe, kujadiliwa na kutolewa uamuzi na tasissi kadhaa za Serikali ambazo kikawaida zinategemea ushauri wa kisheria kutoka katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa serikali na Ofisi za Wakili Mkuu wa serikali kufanya maamuzi...

Ni ngumu kwa ofisi hizo mbili kutoa ushauri kwa hizi tasisi za Serikali kupitisha ama kuruhusu muungano kati ya kampuni hizo za cement ambao Jaji wa Mahakama Kuu pamoja na Wakili Mkuu wa Serikali kwa pamoja wamekubaliana mchakato huo ni batili na umeendeshwa na tume ya Ushindani kinyume na sheria za nchi.

Maamuzi ya Jaji Maghimbi, ni pigo jingine katika mchakato wa kampuni hizo mbili za cement zinazo azimia kuungana kupitia mchakato ulioanza toka mwaka 2017 bila mafanikio.

Afrisam inamiliki asilimia 68 za Tanga Cement ambazo ilitaka iziamishe kwa njia ya mauzo kwenda kampuni ya Scanscem International DA, inayomiolikiwa na Kampuni ya kimataifa ya Heidelberg Group, kwa gharama ya Sh.billion 137 (Dola za kimarekani milioni 55).

Hata hivyo baada ya uamuzi wa Jaji Maghimbi kutolewa, Imani Muhongo ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na uchambuzi wa masuala ya fedha cha Kampuni ya ALPHA CAPITAL alikaririwa na gazeti la serikali la Daily News akieleza kuna uwezekano mkubwa mchakato wa muungano kati ya kampuni hizo kutofanikiwa.

Kwa upande wa pili, Mwenyekiti wa bodi ya Tanga Cement , Lawrence Masha alitoa kauli kwa vyombo vya habari akisema Heildeberg Cement na Afrisam bado wanaangalia namna ambazo mchakato wao kuungana utafanikiwa japokuwa uamuzi wa Baraza Ushindani umefanya mchakato huo kuwa mgumu zaidi kufanikiwa.

Kwa kukumbusha kuhusu historia ya mchakato wa muungano kati ya Twiga Cement na Tanga Cement ni kwamba Aprili 6, 2022 Tume ya Ushindani(FCC) ilitoa ruhusa kwa maombi ya kuungana kibiashara (merger) kati ya kampuni ya Scancem (Maarufu kama Twiga Cement) na Tanga Cement.

Baada ya maamuzi hayo kampuni ya Chalinze Cement ililikata rufani dhidi ya maamuzi hayo mbele ya Baraza la Ushindani ambapo mnamo Septemba , mwaka 2022 Baraza hilo lilibatilisha na kufuta maamuzi ya Tume ya Ushindani ya kuruhusu muungano huo tajwa.

“Kwa kuzingatia kifungu cha11(1) cha Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003, baada kuuweka kando na kuufutilia mbali uamuzi wa FCC, Baraza hili linatoa katazo la kisheria juu ya muungano kati ya Scancem International DA na Tanga Cement,” iliamua Baraza la Ushindani (FCT).

Kwenye shauri hilo rufani, wakata rufani (Chalinze Cement), waliweka pingamizi kwamba Muungano kati ya kampuni hizo mbili kubwa za Cement (Saruji) Tanzania, utavunja Sheria ya UShindani (The Fair Competition Act,2003) ambayo imeweka katazo cha ubia wowote usizidi kiwango cha juu cha asilimia 35 ya hisa ya soko ili kuhakikisha ushindani wa haki.

Ila muungano kati ya kati ya kampuni ya Scancem (Maarufu kama Twiga Cement) na Tanga Cement. Utaipa Twiga Cement asilima 47.27 ya hisa ya soko ambacho ni kikubwa zaidi na matakwa ya shaeri ya Ushindani ya mwaka 2003.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad