HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 28, 2023

KAMPENI YA KUTOA, KUDAI RISITI HALALI YAZINDULIWA NA TRA LEO

Meneja Msaidizi wa ukaguzi TRA Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Thoddy Beyanga akibandika stika katika Duka la Vyombo vya Kieletroniki la Boss jijini Dar es Salaam leo Agosti 28, 2023 wakati wa uzindua wa kampeni ya kuhamasisha wafanyabiasahara kutoa risiti na wananchi kudai risiti za EFD kulingana na kiwango halisi ulicholipia bidhaa halali kwa maendeleo ya Taifa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Boss Shopping Centre, Hanif Janmohamed. 

Meneja Msaidizi wa ukaguzi TRA Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Thoddy Beyanga akizungumza na waandishi wa habarileo Agosti 28, 2023 kabla ya kuzindua stika maalum za kuhamasisha wafanyabiasahara kutoa risiti na wananchi kudai risiti za EFD kulingana na kiwango halisi ulicholipia bidhaa halali kwa maendeleo ya Taifa. Afisa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Isihaka Sharif 
Meneja Msaidizi wa ukaguzi TRA Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Thoddy Beyanga akibandika stika katika Duka la Dawa la JD jijini Dar es Salaam leo Agosti 28, 2023 wakati wa uzindua wa kampeni ya kuhamasisha wafanyabiasahara kutoa risiti na wananchi kudai risiti za EFD kulingana na kiwango halisi ulicholipia bidhaa halali kwa maendeleo ya Taifa. Kushoto ni Afisa Kodi Msimamizi wa Kitengo cha Mashine za EFD, Basya Kubetta.
Meneja Msaidizi wa ukaguzi TRA Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Thoddy Beyanga na Afisa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Isihaka Sharif wakionesha moja ya stika leo Agosti 28, 2023 kabla ya kuzindua stika hiyo maalum za kuhamasisha wafanyabiasahara kutoa risiti na wananchi kudai risiti za EFD kulingana na kiwango halisi ulicholipia bidhaa halali kwa maendeleo ya Taifa. 

Na Avila Kakingo, Michuzi TV
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA, Mkoa wa Kikodi wa Kariakoo wamebandika stika maalumu kwaajili ya uzinduzi rasmi wa kuhamasisha wafanyabiashara kutoa risiti pale wanapouza bidhaa zao na wananchi kudai risiti ambayo itakuwa thamani sawa na bidhaa waliyonunua kwa maendeleo ya Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja Msaidizi wa ukaguzi TRA Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Thoddy Beyanga amesema kuwa kampeni hiyo itakuwa maalumu kwaajili ya kuhamasisha matumizi mazuri ya mashine za kieletroniki (EFD) kwa wafanyabiashara nchini.

"Unapouza toa risiti na vile vile unaponunua bidhaa udai risiti yako."

Amesema kuwa wamebaini kuporomoka kwa utoaji wa risiti kwa sababu risiti zinazotolewa zimekuwa tofauti na matarajio nayo inapelekea makusanyo kushuka.

Beyanga amefafanua faida za kutoa na kudai risiti pale biashara inapofanyika kuwa inasaidia kutunza kumbukumbu, inasaidia katika ukadiliaji wa mapato yanayoendana na uhalisia wa biashara ambayo mfanyabiashara amefanya pamoja na kuchangia pato la taifa.

Amesema kampeni ya uhamasishaji wa wafanyabiashara kutoa risiti na wananchi kudai risiti ni endelevu hivyo jamii inatakiwa kutekeleza bila shuruti.

Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Boss Shopping Centre, Hanif Janmohamed amesema kuwa amejisikia vizuri kwa TRA kuendelea kuhamasisha wafanyabiashara kulipa kodi kwa kutoa risiti halali kulingana na bidhaa iliyonunua.

"TRA sasa hivi wanafanya vizuri, hakuna Harasment kama zilizokuwa zamani, sasa hivi maisha yanakwenda vizuri, pia tunaelimishana kwenye sehemu ambazo zinachangamoto." Amesema Janmohamed

Pia ametoa wito kwa wafanyabiashara kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi pia amesema kuwa kutoa na kudai risiti ni wajibu wa kila mmoja kwa maendeleo ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad