IAA yajidhatiti kutoa wataalam wenye weledi - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 7, 2023

IAA yajidhatiti kutoa wataalam wenye weledi

 

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza na waandishi habari katika banda la IAA  kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

*Waanzisha  Kozi Nne mpya za Shahada 

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
CHUO cha Uhasibu Arusha (IAA) kimesema kuwa kimejidhatiti katika kutoa wataalam kada mbalimbali ikiwemo  fedha katika kuchochea maendeleo ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Chuo hicho katika maonesho ya kimataifa ya kilimo Nane Nane yanayofanyika katika viwanja Vya John Mwakangale jijini Mbeya.

 Profesa Eliamani  Sedoyeka amesema kuwa chuo hicho kiko chini ya Wizara ya Fedha ambapo kimejikita katika kutoa wataalam wa uhasibu na mipango na maeneo mengine yanayofanana.

Amesema kuwa katika maonesho ya Nane Nane wamekuja na kozi mpya Nne za Shahada ambazo ni  Uhasibu wa Fedha(Accountancy and Finance),Usimamizi wa Nyaraka na Taarifa (Records and Information Menagement ),Ukaguzi wa hesabu na Uhakikisho Bima(Auditing and Assurance ), Media Anuwai na Mawasiliano kwa Umma (Multimedia and Mass Communication).

Profesa Sedoyeka amesema kuwa katika Chuo cha Arusha kimeboresha miundombinu ya kufundisha ambapo wanafunzi wanaweza kusoma kwa njia mbalimbali ikiwemo kusoma mtandaoni.
Aidha amesema kuwa Chuo cha IAA kutokana na kuwa na ubobevu wa masuala ya fedha hivyo wataalam hao wanaozalishwa wanajengwa kwa maadili pamoja weledi.

Amesema katika kuendeleza vijana katika biashara na ujasiriamali chuo kimetenga milioni 100 ambazo zinatumika katika kuendeleza ubunifu wa vijana hao na kufuatilia kwa mwaka mmoja baada ya kuhitimu.

Hata hivyo  amesema Chuo kinaendelea  kutanua matawi yake na kwa sasa wanatarajia kuanzisha tawi jipya Mkoa wa Ruvuma  baada ya kuwa na Matawi ,Manyara ,Dodoma na Dar es Salaam pamoja na Arusha ambayo ni Makao Makuu ya Chuo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad