GF TRUCKS & EQUIPMENT YAIBUKA MSHINDI MAONESHO YA MADINI RWANGWA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 27, 2023

GF TRUCKS & EQUIPMENT YAIBUKA MSHINDI MAONESHO YA MADINI RWANGWA

 

Kampuni ya Gf Trucks & Equipment’s Ltd ya jijini Dar es Salam imeibuka mshindi wa Pili wa Banda Bora kwa makampuni yanayotoa huduma ya uuzaji wa mitambo na magari Migodini .

Hayo yamebainika wakati wa kuhitimisha Maonyesho ya Madini na Uwekezaji yaliofanyika Rwangwa mkoani Lindi yalioanza tarehe 21 na kuhitimishwa na Waziri mkuu Kasimu Majaliwa aliye ambatanana na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambae alikua mgeni Rasmi

Akizungumza wakati wa ufungaji wa Maonyesho hayo Kikwete alisema Wakati anastaafu aliiacha Rwangwa ikiwa haiku hivi na amekuja ameikuta Rwangwa ile nah ii ya sasa ni Mbingu na Aridh kutokana na uwe,kezaji wa madini na fursa zilizopo mkoa wa Lindi kwenye Madini hivo mabadiliko ni makubwa mmno.

Nae Afisa Mauzo wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Peter William alisema wao kama Gf wamejikita kuhakikisha wanawakomboa wachimbaji wa dogo na wakati kwa kuanzisha mapango maalumu wa kuhaikisha wanawawezesha wachimbajinchini kupata mitambo ya kuchimbia kwa gharama nafuu kwa kushirikiana na tasisi za Kibenki wameazisha utaratibu wa kumkopesha mashine (matambo )iki kuweza kufanya kazi kwa uharaka Zaidi.


Pia Peter alisema wamejipanga kuwekeza nguvu Zaidi na hivi karibuni watafungua ofisi katika ukanda wa kusini ili wateja wasipate usumbufu wa kuja hadi Dar es salaam.Kampuni ya Gf inayojishungulisha na uuzaji wa Magari ya FAW, FORLAND,HONG YANG (trucks) pamoja na mitambo ya XCMG maalumu kwa shuguli za migodini na Wakandarasi wa Barabara.

Akihitimisha maonyesho hayo Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa onyo kwa maafisa wanaohusika na utoaji wa leseni za madini kuacha tabia ya kuwazunguka wananchi wanaokwenda katika ofisi zao kuomba leseni za uchimbaji baada ya kubaini uwepo wa madini kwenye baadhi ya maeneo na kisha kuwapa wachimbaji wengine.

”…Acheni tabia ya kuwaonea wananchi wanaotoka kwenye maeneo yenye fursa ya madini anakuja kuomba leseni ya kumiliki eneo hilo na unamwambia aache taarifa zake aje kesho kuchukua majibu akija kesho unamwambia eneo hilo limeshachukuliwa na mtu mwingine kumbe wewe unamtafuta mtu wa kuweza kumiliki ili upate chochote kitu, tukikugundua hatua kali zitachukuliwa dhidi yako. ”
Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Agosti 26, 2023) wakati akifunga Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji mkoani Lindi yaliyofanyika kwenye viwanja vya soko la Kilimahewa wilayani Ruangwa. Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha uwepo wa mazingira bora kwa wawekezaji wa ndani na nje.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameuagiza uongozi wa Wakala wa Jiolojia Tanzania ufanye tafiti za madini za kimkakati kwa kushirikiana na halmashauri kwa lengo la kuwasaidia Watanzania kufanya shughuli zao kwa tija na kuhakikisha mipango sahihi ya matumizi ya ardhi inafikiwa.

Afisa  Mauzo wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd ,  Peter  William  akiwa ameshikilia Zawadi ya Tuzo kwa kuwa kampuni ya pili kwa utoaji wa uuzaji wa magari na mitambo migodini wakati wa maonyesho ya madini Rwangwa
Banda bora
Tuzo
 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad