DC MATINYI AWAPONGEZA TEJA KUUNGANISHA WAKIMBIAJI BARA NA VISIWANI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 27, 2023

DC MATINYI AWAPONGEZA TEJA KUUNGANISHA WAKIMBIAJI BARA NA VISIWANI

 

DC wa Temeke, Mhe. Mobhare Matinyi, akizungumza na wakimbiaji baada ya kumaliza jogging iliyoandaliwa na TEJA.
DC Matinyi akikabidhi cheti.
DC alimpa cheti mwakilishi wa moja ya klabu zilizoshiriki. Kushoto ni Mwenyekiti wa TEJA, Rashid  Pazzi.

DC Matinyi na viongozi wa TEJA wakikimbia kwa mwendo wa polepole kutoka daraja la Mwalimu Julius Nyerere, Kigamboni, hadi Uwanja wa Uhuru ambao ni umbali wa km 6.
DC Matinyi kushoto akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa TEJA, Janet Maseke, wakati wa mazoezi ya viungo baada ya kumaliza mbio za nwendo wa polepole (jogging)

Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
MKUU wa Wilaya ya Temeke Mhe. Mobhare Matinyi amekipongeza Chama cha Mbio za Mwendo wa Polepole Temeke Jogging Association (TEJA), kwa kuandaa tamasha kubwa lililojumuisha Mikoa 12 ya Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

Tamasha hilo la mbio za mwendo wa polepole wa umbali wa kilomita sita limefanyika leo asubuhi Jumapili Septemba 27 2023 zimeanzia Kigamboni kwenye daraja la Mwalimu Julius Nyerere hadi Uwanja wa Uhuru na kuongozwa mwanzo hadi mwisho na Mhe. Matinyi akiwa na Mwenyekiti wa TEJA Mhandisi Rashid Pazi na Makamu Mwenyekiti Janet Maseke.

Mhe. Matinyi amewapongeza TEJA mbali ya mbio hizo pia wameandaa zoezi la upimaji afya pamoja na uchangiaji damu kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Temeke.

Mhe. Matinyi amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, amesema TEJA imeonesha uanamichezo na uzalendo kwa kuwajali wahitaji wa damu na kuipongeza kauli mbiu ya mwaka huu ya kupiga vita ukatili wa kijinsia kwa watoto, wanawake na kupinga mahusiano ya jinsia moja.

Kabla ya kugawa vyeti kwa wadhamini na washiriki Mhe. Matinyi amewasilisha salamu za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwapongeza washiriki wa 'Jogging' hiyo kwa kujali afya zao kupitia mazoezi, kuchangia damu na kupinga unyanyasaji wa kijinsia.

"Mhe. Mkuu wa Mkoa amenituma niwasilishe salamu za Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan Kiongozi mwanamichezo kwenu nyote washiriki " amesema Mhe. Matinyi.

Katika risala yao TEJA kwa niaba ya mamia ya wakimbiaji wamemwomba Rais Dkt. Samia ashiriki nao katika mbio hizo za mwendo wa pole pole katika siku za usoni.

Aidha Mhe. Matinyi amewasilisha pongezi na shukurani kutoka kwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwa wanamichezo hao kuchangia damu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Pindi Chana kwa wananchi hao kujali michezo na pia kutoka kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima kwa washiriki hao kuunga mkono juhudi za serikali kupiga vita unyanyasaji kwa watoto na wanawake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad