DC KIGAMBONI, BULEMBO AONGOZA MBIO ZA HISANI KITUO CHA JCH, AHIMIZA JAMII KUWA NA UPENDO KWA WATOTO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 6, 2023

DC KIGAMBONI, BULEMBO AONGOZA MBIO ZA HISANI KITUO CHA JCH, AHIMIZA JAMII KUWA NA UPENDO KWA WATOTO

 

Picha ya pamoja.
Mkurugenzi  wa  JCH  Anna Ngoda  akifafanua jambo pamoja na kuwashukuru wahisani , DC  wa.Kigamboni kwa kuungana nao  na watu kutoka kada mbalimbali  waliojitokeza kwenye mbio hizo zilizokua za Km.5,Km10 na Km.21
DC Kigamboni Mheshimiwa  Halima Bulembo  akizungumza  na wananchi na watu wa kada  mbalimbali mara baada ya mbio hizo.

Na Khadija Kalili Michuzi Tv
MKUU wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo ametoa pongezi kwa kituo cha kulelea watoto waliotelekezwa na wazazi wao kinacho fahamika kwa jina la Jerusalem Children's Centre (JCH) , kutokana na jitihada yao ya kuwakusanya watoto hao na kuwapa malezi ya upendo ambavyo wamevikosa huko walikokuwa.

"Awali ya yote nampongeza mwanzilishi wa kituo hiki pamoja na wafanyakazi wa kituo ikiwa ni pamoja na wafadhili ambao wamekua na moyo wa kutunza na kuwahudumia watoto hawa"amesema DC Bulembo.

"Hili jukumu ambalo limechukuliwa na kituo hiki cha Jerusalem Children's Home siyo dogo na linahitaji kuungwa mkono, hivyo basi nawaahidi kuwa nitakuwa sehemu ya msaada katika safari hii ya malezi kwa watoto wetu hawa ambao walikua wakiishi katika mazingira magumu".

"Pongezi zangu zinakwenda sambamba kuwataka msichoke kuwahudumia ili wote kwa pamoja tuweze kulifikia lengo lililotarajiwa na nina imani kubwa tutafika wote kwa pamoja" amesema DC Bulembo .

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho cha Jerusalem Children's Home Anna Ngoda amesema kuwa hivi sasa kituo kinalea na kuhudumia watoto 38 na kina wafanyakazi 8.

"Hii ni Marathon ya pili kufanyika ya kwanza ilifanyika mwaka 2022 ambapo tulipata fedha na zote tumenunua eneo la ardhi ambapo tumepanga ndipo tutajenga makazi ya kudumu ya kituo hapa kigamboni" amesema Ngoda.

Tuna furaha isiyo na kifani kwa jinsi Marathon hii ilivyofana na kupata muitikio tuna imani mwakani itafana maradufu. Msaada kutoka kwa jamii umekua ni mkubwa hivyo nina imani kubwa kuwa kwa pamoja tunaweza kujenga mustakabali wenye matumaini kwa watoto wetu ambao wamekua wakiishi kwenye mazingira hatarishi.

Ngoda amesema kuwa tangu waanze kutoa huduma ya ulezi kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi tayari wamefanikiwa kuwaunganisha baadhi ya watoto na familia na maisha yanaendelea huko waliko.

Mbio hizi zilikua za Km.5 Km. 10 na Km .21 Kituo hicho cha JCH kimezinduliwa Aprili 15,2020 na mbio hizo za hisani zimefanyika leo Agosti 6 2023.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad