BRELA, LGAs ZATAKIWA KURAHISISHA UTOAJI LESENI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 6, 2023

BRELA, LGAs ZATAKIWA KURAHISISHA UTOAJI LESENI

 


WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Mamlaka ya Serikali za Mtaa (LGAs) zimetakiwa kuangalia jinsi ya kurahisisha utoaji wa Leseni wa Leseni za Biashara kundi "A" na "B" ili kuondoa urasimu kwa wafanyabiashara.

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 5 Agosti, 2023 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (Mb), alipotembelea banda la BRELA katika maonesho ya Wakulima ya Kimataifa (Nanenane) yanayofayika katika uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya.

Mhe. Kigahe amesema mfumo wa Tausi wa utoaji wa Leseni za Biashara kundi "B" hausomani na mfumo wa BRELA kupitia Dirisha la Biashara la Taifa (Tanzania National Business Portal -TNBP) wa kutoa Leseni za Biashara kundi "A" hivyo inasababisha usumbufu kwa wafanyabiashara.

"BRELA kaeni na Mamlaka ya Serikali za Mitaa ili muone changamoto hii mnaitatuaje, hiki ni kilio cha wafanyabiashara ambao matarajio yao makubwa kwa Serikali ni kuwaondolea urasimu usiokuwa wa lazima, " amesisitiza Mhe. Kigahe.

Mhe. Kigahe ameongeza kuwa kwa kuanzia maafisa wa BRELA wapite katika mabanda ya Halmashauri yanayoshiriki katika maonesho hayo ili kujifunza jinsi mfumo wa Tausi unavyofanya kazi ili kupata picha halisi itakayowezesha kuwasaidia wafanyabiashara.

Kwa mujibu wa Sheria ya Leseni za Biashara (Sura Na. 208) jukumu la utoaji wa Leseni za Biashara kundi "A" ni la BRELA na kundi "B" ni la Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad