BONDIA WA MUAITHAY SHIJA AITOLEA UVIVU TPBRC - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 9, 2023

BONDIA WA MUAITHAY SHIJA AITOLEA UVIVU TPBRC

 


Na Khadija Seif,Michuzi blog
BINGWA wa Mkanda wa WBC Emmanuel Shija ameiomba Kamisheni ya Ngumi (TPBRC) kuangalia upya sheria na kanuni ya mchezo huo.

Hatua hiyo imetoka baada ya baadhi ya mabondia kucheza mapambano mara Kwa mara bila kujalia afya zao miaka ya baadae.

"Mabondia wanatakiwa kujali afya zao kucheza mara kwa mara mapambano bila kupata muda wa kupumzika ni hatari kwa afya za mabondia kwa baadae kwa sasa ni ngumu kuona athari zake, hivyo niwaombe TPBRC kuangalia upya sheria au kutunga sheria nyingine itakayosaidia kupunguza athari hizo kwa baadae kwa sababu ngumi ni mchezo wa hatari sio wa vichekesho ulingono, "alisema.

Shija ameipongeza Serikali pamoja na Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kuwekeza nguvu kuhakikisha michezo nchini inapewa nafasi kubwa na kushiriki kushuhudia michezo katika sehemu mbalimbali pale matukio yanapoandaliwa.

Pia ameeleza shahuku yake ni kuona mabondia wa mchezo wa ngumi na mateke (Kick boxing) pamoja na Muhaythai wanatambulika nje na ndani ya Tanzania na kuongeza kipato kupitia michezo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad