ALAF yazindua dhamana ya bidhaa kulinda ubora - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 15, 2023

ALAF yazindua dhamana ya bidhaa kulinda ubora

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa dhamana ya bidhaa za ALAF (Warrant) ili kulinda ubora wa bidhaa zake, uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 15, 2023.

SERIKALI imewataka wazalishaji wa bidhaa mbali mbali za chuma nchini kuhakikisha wanazalisha bidhaa zinazokidhi ubora ili kuwawezesha walaji kutimiza malengo yao ya muda mrefu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameyasema hayo leo Agosti 15, 2023 jijini Dar Es Salaam wakati akizindua dhamana ya bidhaa za ALAF (Warrant) ili kulinda ubora wa bidhaa zake.

Amesema kuwa kama kampuni zote zikifuata mfumo huo wa kampuni hiyo basi Tanzania hakuwezi kuwa na bidhaa feki.

Amesema ukosefu wa ubora kwenye bidhaa una athari kubwa za kiafya na usalama kwa walaji ambao wanatakiwa kulindwa.

“Walaji wanatakiwa kuichangamkia dhamana hii ya bidhaa ili wajiridhishe na ubora wa bidhaa na uhalali wake kabla ya kununua,” amesema na kusiistiza kuwa serikali itaendelea kusimamia kwa karibu suala la ubora ili kuhakikisha walaji wanapata kile kilichobora na imara.

Aidha Chalamila, ameipongeza kampuni ya ALAF kwa kuibua mjadala huu wa bidhaa bandia. Alitoa wito kwa vyombo vyote vya usimamizi na wadau wengine wote kuimarisha vita dhidi ya wimbi le vifaa visivyokidhi ubora.

Pia ametoa wito kwa taasisi mbalimbali kama vile TBS, FCC, OSHA na nyinginezo kuhakikisha wazalishaji wanazingatia ubora ili kuwalinda walaji.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa ALAF, Isamba Kasaka, amesema lengo la uzinduzi wa dhamana ya bidhaa za chuma na bidhaa nyingine za ALAF ni kuwapa amani wateja wetu kuwa wamefanya chaguo sahihi la kuezeka na kutumia bidhaa za ALAF, kwani wanaamini kujenga nyumba moja ya hatua mhimu sana kwenye maisha ya wateja.

Pia amesema dhamana hiyo mpya inalenga kuwahakikishia ubora kuhusu bidhaa za ALAF ambazo ni pamoja na mabati na nondo.

Amesema ALAF imeendelea kushtushwa na wimbi la bidhaa za chini ya kiwango na bidhaa bandia ambazo zinaathiri sekta zote nchini.

Amesema kupitia programu hiyo ya dhamana bidhaa wataendelea kutoa elimu kuhusu bidhaa za chini ya kiwango na feki.

“Tunafanya kazi kwa karibu na serikali, vyombo vya kuimarisha sheria na vyombo vya uthibiti ili kukabiliana na wimbi hili la bidhaa feki,” amesema.

"Ili kupata thamani ya nguvu wanazotumia na fedha walizowekeza wanahitaji bidhaa bora na inayokidhi viwango vilivyowekwa na shirika la viwango nchini." Amesema

Amesema dhamana hiyo itakuwa ya miaka 15 na itatolewa kwa kila manunuzi yatakayofanyika katika Kiwanda na kupitia mawakala wote wa kiwanda hicho waliopo kwenye mikoa zaidi ya ya mitano nchini.

Amesema tangu kuanzishwa kwake kampuni ya ALAF imekuwa ni chachu na maendeleo na utafiti katika teknolojia ili kuhakikisha tunampatia mteja bidhaa yenye ubora wa hali ya juu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akikata keki mara baada ya  uzinduzi wa dhamana ya bidhaa za ALAF (Warrant) ili kulinda ubora wa bidhaa zake, uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 15, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila na viongozi mbalimbali wakishangilia mara baada ya kuzindua dhamana ya bidhaa za ALAF (Warrant) ili kulinda ubora wa bidhaa zake, uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 15, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akizungumza wakati wa  uzinduzi wa dhamana ya bidhaa za ALAF (Warrant) ili kulinda ubora wa bidhaa zake, uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 15, 2023.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad