HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 9, 2023

XCMG YATIMIZA MIAKA 80 SOKONI IKIJA NA OFFA YA SABASABA KWA WATEJA

 

Kampuni ya Gf Trucks & Equipment’s Ltd ya jijini Dar es Salam imewataka wadau wa sekta ya Ujenzi ,Wakandarasi , na wadau wa madini pamoja na wafanya biashara sekta ya usafirishaji nchini kuchangamkia punguzo la bei kwa mashine na magari (trucks )yanayouzwa na kampuni hiyo ndani ya viwanja vya sabasaba

Akizungumza na Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina wakati alipotembelea banda lao ndani ya viwanja vya Maonyesho ya 47 ya Biashara ya kimataifa.

Afisa masoko Mwandamizi wa kampuni ya GF, Poul Msuku alisema kampunin ya GF imeamua kuwashika wadau woote katika sekta ya Madini na Ujenzi kwa kuhakikisha ipo karibu yao kila siku kwa kutengeneza mpango maalumu utakaowasaidia kupata Mitambo hiyo kwa Gharama nafuu na kumfikishia mteja hadi nyumban kwake.

Unajua GF ni wakala wa wauzaji wa mitambo ya XCMG nchini na kuzingatia hilo hivi sasa XCMG imetimiza miaka 80 ya kutoa sokoni hivyo ni kampuni iliyokubalika duniani kote katika sekta ya uchimbaji kwani wna mitambo ya mikubwa na yenye teknolojia ya kisasa hivyo katika kutambua hilo tumeamua kuwa na offa kwa wteja wetu huku tukisherehekea miaka 80 na sabasaba kwa pamoja tunajambo kwa wateja.

Poul aliendelea kusema GF inampango maalumu kwa kushirikiana na Tasisi za kifedha (mabenki)wameanzisha mpango wa kumkopesha mteja mwenye mradi mitambo kwa kuzingatia makubaliano maalumu baina ya mteja na beki huku vigezo na mshariti vikizingatiwa

Mpango huu hasa unawalenga wakandarasi na wachimbaji wazalendo lengo likiwa ni kuwasaidia kuweza kushindana na makampuni makubwa ya kigeni
Nae Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina aliwataka wachimbaji kuchangamkia fursa hiyo kwani ni makampuni machache wanaoweza kuwakumbuka na kuwapatia mitambo kwa staili hiyo apo awali .

FEMATA kupitia STAMICO waliingia makubaliano na kampuni ya GF Trucks ya kuhakikisha wanashirikiana katika kuhakikisha wachimbaji wanakwamuliwa kwa kupatiwa vitendea kazi kwa gharama nafuu,Hivyo aliwapongeza GF na kuwataka kuendelea kufungua ofisi sehemu zoote zenye migodi ili wwachimbaji waweze,kiuchangamkia fursa

Mpaka sasa kampuni hiyo imefungua ofisi katika maeneo mbali mbali nchini ukanda wa kusini yaani mikoa ya Ruvuma na Mbeya ,kanda ya ziwa wanapatikana Geita na wako mbioni kufungua ofisi Chunya alimaliza Poul toa punguzo maa lumu kwa wateja wetu ambao watatembelea banda letu lililopo katika maonyesho ya sabasaba

Akifafanua zaidi punguzo hilo la bei (sabasaba special) limelenga zaidi katika mitambo inayotumika kwa shunguli za ujenzi (XCMG Motor grade) ambapo wakandarasi wazalendo wenye miradi ya ujenzi hii ndio fursa yao kwani mwaka mpya wa seriklali ndio huu na wakandarasi wazalendo nio kipamumbele katika hili

Pia wanunuzi na wadau wakubwa wa mitambo hii ni Makampuni ya Ujenzi,Makandarasi pamoja na wamiliki wa migodini,Pia tuna magari makubwa ya mizigo FAW,HONG YANG (trucks) pamoja na tipper zinazotumika katika shunghuli mbalimbali zikiwepo machimbo ya mchanga na katika baadhi ya halmashauri zimekuwa zikitumiwa kwa kukusanyia takata na shughuli nyingine.

Akienda mbali zaidi Lukolo alitanabaisha magari hayo ya FAW na HONG YANG Kwa sasa yaliotengenezwa na kiwanda cha GFA kinachomilikiwa na watanzania kilichopo Kibaha mkoani Pwani hivyo katika maonyesho ya mwaka huu tunajivunia kuonyesha magari yaliotengenezwa na wataalamu wetu wakishitikiana na wataalamu kutoka nje.


Waziri mkuu Kassimu majaliwa akiwa ameambatana na Waziri mku mstaafu Mizengo Pinda wakipita jirani mitambo ya XCMG ndani ya banda la kampuni ya GF wakati akikagua mabanda katika maonyesho ya biashara ya 47 ya kimataifa jijini Dar es salaam.

Afisa mauzo mwandamizi wa kampuni ya GF Trucks & Equipment's Ltd Poul Msuku akimwelezea Rais wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina  wakati alipotembelea katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es salaam

Pou Msuku akizungumza na wawakilishi wa EXMG kutoka China kuhusu maonyesho  namadhimisho ya miaka 80 ya XCMG sokoni

Moja ya mtambo wa kutengenezea barabara motor greda


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad