WAZIRI DKT. ASHATU KIJAJI ASISITIZA USIMAMIZI WA USAHIHI WA VIPIMO AKIZINDUA BODI MPYA YA USHAURI WMA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 27, 2023

WAZIRI DKT. ASHATU KIJAJI ASISITIZA USIMAMIZI WA USAHIHI WA VIPIMO AKIZINDUA BODI MPYA YA USHAURI WMA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) asisitiza bodi  mpya ya ushauri ya Wakala wa Vipimo kuhakikisha walaji wanalindwa kupitia uhakiki wa vipimo ili wanaponunua bidhaa mbalimbali  wapate kuona  thamani ya fedha  katika bidhaa wanazonunua.  

Dkt.Kijaji ameyasema hayo Jijini Dodoma leo tarehe 27 Julai, 2023 alipokuwa anazindua bodi ya sita ya ushauri ya Wakala wa Vipimo.

Aidha, amemshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala pamoja na wajumbe   kwa kuaminiwa  na kuteuliwa kwani  wanaunda timu bora na inayotoa  matumaini makubwa katika kuendelea kusimamia matumizi sahihi ya Vipimo kwenye bidhaa pamoja na vifungashio vyake ili watumiaji waweze kupata kile walichokilipia. 

Pia, ameitaka bodi kufanya kazi yake kwa weledi na kuhakikisha inasimamia usalama wa mali za watanzania kupitia vipimo sahihi ambapo  matarajio ya Serikali ni kwamba wataisaidia wakala  katika kuhakikisha inatekeleza vipaumbele vya serikali kwenye usimamizi wa matumizi sahihi ya vipimo nchini, na kupitia usimamizi huo wataweza kuwahudumia wafanyabiashara na wawekezaji  na kuishauri serikali kuhusu masuala yote yanayohusu vipimo na kuhakikisha wakala inamlinda mlaji kwa kutumia vipimo sahihi Dkt. Kijaji amesema.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Kijaji  ameitaka wakala  kuwa pamoja na kazi nzuri wanayoifanya ya usimamizi wa vipimo ni vyema  kuendelea kuongeza nguvu katika  kusimamia usahihi wa vipimo  kwenye maeneo mbalimbali

Naye Mwenyekiti wa Bodi  ya Wakala wa Vipimo, Dkt. Eliza Alfred Mwakasangula alimshukuru Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), pamoja na Menejimenti  ya Wakala kwa kuahidi  kusimamia  na kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na kushauri Wizara ipasavyo kwenye masuala ya vipimo ili kuhakikisha wakala inaendelea kutoa huduma bora kwa Wananchi inao wahudumia.

Wakati huohuo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Bi. Stella Kahwa amemshukuru Waziri kwa kuteua Bodi ambayo itasaidia kuleta maendeleo  kwa wakala, ikiwa ni pamoja na  kuongeza idadi ya vipimo vinavyohakikiwa kwa mwaka na kuhakikisha Wakala inaendelea kuchangia katika mfuko mkuu wa Serikali ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad