Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Utumishi wa Umma na Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 17 hadi Julai 22, 2023.
Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Utumishi wa Umma na Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho (Watatu kutoka kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa Chuo Cha Utumishi wa Umma katika Maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 17 hadi Julai 22, 2023.
Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Utumishi wa Umma na Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho akizungumza na mmoja ya wananchi aliyetembelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam panapofanyika Maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu yaliyoanza Julai 17 hadi kutamatishwa Julai 22, 2023.
Na Mwandishi wetu
KAIMU Makamu Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Ernest Mabonesho ametoa wito kwa jamii kukitumia Chuo cha Utumishi wa Umma katika kufanya tafiti tumizi ili kutatua changamoto zinazozikabili taasisi za Umma na taasisi binafsi.
Hayo ameyasema wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 18, 2023 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambako kunafanyika Maonesho ya 18 ya Vyuo Vikuu ambayo yalianza Julai 17 hadi Julai 22. Amesema watumie chuo hicho kwa manufaa ya jamii nzima.
Amesema jamii itembelee Banda la Chuo hicho ili waweze kufanya tafiti kwa kusaidiana lakini pia kama jambo ambalo linahitaji ushauri wafike ili kupata ushauri wa maeneo yanayohitaji tafiti kwaajili ya kutatua changamoto za jamii.
"Karibuni sana sisi tunafanya Consultance kwa manufaa ya utumishi wa umma, kwaajili ya manufaa ya Tanzania ili kumsaidia Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwaajili ya kuongoza nchi kwa mwelekeo anaoutaka yeye." Amesema
Lakini pia wanatoa mafunzo mbalimbali kama mafunzo ya maadili, Huduma kwa wateja ambayo ni huduma muhimu kwani bila huduma hiyo hawawezi kwenda kwa sababu wanamwona mteja kuwa ni koo la kila kitu yaani yupo katikati ya shughuli zote za kiutumishi na hata zile ambazo sio za kiutumishi.
Dkt. Mabonesho amesema kuwa wanafundisha namna ya kuenzi tunu za taifa, namna ya kuweka siri za serikali lakini pia siri ya watumishi wa umma yaani wateja wake ambao watakuwa wanaenda kwenye ofisi za Umma na binafsi hivyo huwaangalia kwenye maeneo hayo kwasababu maeneo hayo ndio muhimu.
"Lakini zaidi ya yote tukumbuke kwamba chuo cha utumishi wa umma wakati kinaanzishwa kilikuwa na lengo la kuwajengea uwezo watumishi na kwamba tunaamini watumishi ni rasilimali kubwa ya taifa rasilimali ziko nyingi lakini vyote hivyo vinatengenezwa na mtu kwahio tunapomwandaa anaweza kusimamia rasilimali zote.
Kwahiyo wanachokifanya ni kumpa uwezo (Soft skills) ya kuweza kuzitumia zile rasilimali zilizopo ili ziweze kuwa na manufaa kwa watanzania wote na manufaa kwa dunia nzima.
"Lakini pia tunatoa mafunzo kwa viongozi watarajiwa yaani ambao wapo kwenye 'level ya senior paka Principal' tunagemea hawa wanakaribia uteuzi hivyo tunawaandaa ili watakapo fikia uteuzi basi wasipate tabu kufanya kazi sawasawa na nafasi zao lakini.pia tunaenda na utaratibu huo mpaka mtu anapokaribia kustaafu tunamwandaa mtumishi anaenda kustaafu baada ya kuacha Utumishi wa Umma anaingia kwenye sehemu nyingine ambako kuna maisha tofauti kidogo.
Amesema Chuo hicho kinamwandaa kisaikolojia mtumishi wa Umma anapoanza kazi, anapo karibia kustaafu pia hutoa mafunzo ya namna mtumishi huyo kujitafutia kipato chake cha kila mwezi ili kuendana na kipato chake pale anapostaafu kwani atakuwa anategemea Pensheni tuu.
Dkt. Mabonesho akizungumzia kuhusiana na Matawi waliyonayo amesema kwasasa wanamatawi sita ambayo ni Dar es salaam, Tanga, Singida, Tabora, Mbeya na Mtwara.
Amesema Chuo hicho ni chuo cha zamani kwasababu ukiangalia historia yake kilianzishwa mwaka 1963 wakati huo kinaitwa Civil Service Taining Centre yaani chuo cha watumishi wa serikali cha mwaka 1963 lakini pia kikaungana na chuo kingine cha uhadhiri ambapo kilianza rasmi1972.
No comments:
Post a Comment