VIONGOZI WA DINI KUWA MABALOZI WA ELIMU YA LISHE KWA WAUMINI MKOANI MBEYA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 26, 2023

VIONGOZI WA DINI KUWA MABALOZI WA ELIMU YA LISHE KWA WAUMINI MKOANI MBEYA

 VIONGOZI wa Dini Mkoani Mbeya wametakiwa kutoa Elimu ya lishe bora kwa waumini wao kwa lengo la kuhamasisha matumizi bora ya chakula na kuwa na afya bora ili kuleta maendeleo ya kiuchumi kitaifa na jamii kwa Ujumla


Hayo yanajiri wakati Mganga Mkuu wa mkoa wa Mbeya Dkt Maisara Karume akifungua Mkutano wa wadau wa masuala ya lishe na viongozi wa dini Ulioratibiwa na wizara ya afya kwa Kushirikiana na Shirikla lisilo la kiserikali la Helvetas Mkoani Mbeya.

“. Sote tunajua kuwa ili tuweze kuleta maendeleo na kufikia uchumi wa viwanda katika nchi ni muhimu tuwe na Taifa la watu wenye lishe na afya bora.” Alisisitiza Karume

Katika Hotuba yake Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha Lishe Wizara ya Afya Neema Joshua amesema lengo la kuwashirikisha viongozi wa dini ni kutengeneza Jumbe za kuelimisha waumini hao kwa kuangalia mahusiano ya maneno yaliyoandikwa kwenye vitabu vya kiimani ili waumini waweze kusikia na kuamini madhara yatokanayo na ukosefu wa Lishe bora.

Nao baadhi ya Viongozi wa dini akiwemo Mch.Yared Nkoswe Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Nyanda za Juu Kusini amesema kanisa limewekeza nguvu kubwa katika masuala ya afya.

Utapiamlo wa aina yoyote huchangia kwa kiasi kikubwa kiwango cha umaskini kwa kuongeza uwezekano wa kupata magonjwa, vifo, kudhoofisha makuzi na maendeleo ya mtoto yanayosababisha uzalishaji, utambuzi, na maamuzi duni wakati wa utu uzima.

Ikumbukwe kuwa Takwimu za Kitaifa za sasa zinaonyesha kuwa 30% ya watoto wenye umri chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa, wakati 12% wana uzito pungufu, na 3% wana ukondefu hii ni kwa mujibu wa utafiti mkubwa wa kidemografia wa masuala ya afya na lishe (TDHS,2022).

Bi.Neema ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutoa elimu ya lishe katika jamii kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo ya dini ili kuleta mabadiliko chanya ya tabia za Lishe katika jamii yetu.

“Uamuzi huu umezingatia umuhimu na nafasi mliyonayo viongozi wa dini katika kuhakikisha jamii yenye afya na usitawi bora kwa kuzingatia nafasi yenu ya uongozi na mamlaka ya kiroho, viongozi wa dini mna fursa ya kuwa nguvu ya mabadiliko katika maisha ya waumini kwa kuwapa mwongozo, elimu, na ushauri juu ya lishe bora na afya kwa ujumla. Alieleza Bi Neema

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad