TAA yaweka mikakati ya ujenzi wa viwanja vya ndege nchini - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 5, 2023

TAA yaweka mikakati ya ujenzi wa viwanja vya ndege nchini

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura  akionesha mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege Msalato Dodoma   kwenye  maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa  Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage  Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura  akihudumia wananchi waliotembelea banda la TAA kwenye  maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa  Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage  Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura  akihudumia wananchi waliotembelea banda la TAA kwenye  maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa  Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage  Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
*Filamu ya Royal Tour ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan yachochea idadi ya wageni kuingia nchini.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), imesema imeendelea kujenga viwanja vipya na kuboresha vya zamani ili kupokea wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini kuwa na uhakika usafiri na usafirishaji wa budhaa zinazozaliswa ndani ya nchi hali itakayosaidia kuendelea kukuza uchumi wa nchi.

Hayo ameyasema Mkurugenzi Mkuu wa TAA Mussa Mbura kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba.

Mbura amesema kuwa Mamlaka hiyo imekasimiwa kuendesha na kusimamia viwanja vya ndege 58 Tanzania Bara.

"Vipo Viwanja vikubwa ambavyo vimekuwa vukitumiwa kwa kusafirisha abiria kutoka ndani na nje ya nchi, ikiwemo Kiwanja Cha Mwalimu Juliaus Kambarage Nyerere kilichopo jijini Dar es Salaam.

Amesema Kauli Mbiu inayosema Tanzania :Ni mahali sahihi biashara na Uwekezaji,kwa sababu wawekezaji ili waweze kuja nchini lazima watumie viwanja vya ndege na ni asilimia 60 kufika nchini kwa kutumia Viwanja hivyo.

"Baada ya ugonjwa wa UVICO 19,tunapokea wageni,wawekezaji wanaoingia nchini na kwa kulitambua hilo Serikali yetu ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha Viwanja vipya na kwa sasa tuna mradi mkubwa unaendelea Msalato Dodoma kwenye Makao Makuu ya Nchi.

"Kufuatia filamu yetu ya. Royal Tour imefanya wageni wengi waweze kuja kwa ajili ya kuangalia vivutio mbalimbali vilivyopo nchini.

"Viwanja vilivyopo nchini ni salama pamoja na kuwepo kwa Taa katika kurahisisha wasafiri kusafiri na ndege kutua na kuruka muda wowote," amesema Mbura.

Mbura amesema Watanzania na waonyeshaji katika maonesho ya sabasaba wafike katika banda wapate elimu na huduma zitolewazo na Mamlaka hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad