Shule ya St Mary Goreti yasifiwa kwa mchango wake katika jamii - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 8, 2023

Shule ya St Mary Goreti yasifiwa kwa mchango wake katika jamii

 

MBUNGE wa Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro Priscus Tarimo, ameupongeza uongozi wa shule ya sekondari ya St Maria Goreti kwa mchangao wao mkubwa unayotoa katika kukuza sekta ya elimu na jamii kwa ujumla

Tarimo ametýoa pongezi hizo wakati wa kambi maalum ya kupima afya na kuchangia damu iliyoandaliwa na uongozi wa shule hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yanayooendelea ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.

“Shule hii ilianza kama shule ya sekondari ya kawaida, baadaye ikawa ya hadi kidato cha sita; sasa hivi uongzi wa shule hii umeanzisha shule ya awali pamoja na ya msingi, haya ni mafanikio makubwa kwa shule yenu na mchango mkubwa katika kukuza sekta ya elimu hapa nchini”, amesema.

Aidha aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuchangia maboresho ya mazingira mkoani Kilimanjaro kwa kuchangia miche ya miti na uandaji wa miti katiak wilaya zote za Mkoa kama sehemu ya maadhimisho.

“Nimeelezwa ya kuwa mmechangia miti 2,000 itakayopandwa maeneo mbalimbali hapa mkoani Kilimanjaro, huu ni mchango mkubwa katika kuboresha mazingira haswa ikitiliwa maanani ya kuwa moja wapo ya ajenda za serikali ni kuhakikisha mazingira yanaboreshwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi”, ameongeza Tarimo

Kuhusu kambi hiyo, Tarimo amesema pia ni njia nzuri kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya miaka 25 ya shule ambapo amesema wananchi watapata fursa ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wananchi wengine sambamba na kupima hali zao za afya bure.

Tarimo ambaye katika hafla hiyo alijisajili kama mshiriki wa mbio zilizoandaliwa kama sehemu ya maadhimisho hayo, pia ameupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuandaa mbio hizo ambazo zitachangia kuboresha maisha ya washiriki sambamba na kukuza sekta ya michezo.

Mapema, akimkaribisha Mbunge huyo kutoa salamu zake, Mkuu wa shule ya sekondari ya St Maria Goreti Sista Clementina Kachweka, alisema kambi hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kuchangia damu kwa wahitaji, haswa ikitiliwa maanani mahitaji ya damu yamekuwa ni makubwa katika taasisi za tiba mkoani Kilimanjaro.

“Mbali na kuchangia damu, pia watu watapata fursa za kupima afya zao bure, lengo ni kuwapa watu kuweza kujua hali zao za kiafya na pale anapogundulika kuwa na maradhi aweze kuanza tiba mapema”, alisema.

Aidha, sista Kachweka ameuishukuru hospitali ya KCMC ya Moshi kwa kuwa mstari wa mbele katika kuratibu zoezi hilo la upimaji afya na kuchangia damu huku wakisaidiwa na wataalamu wengine kutoka Hospitali ya St Joseph, Hospitali ya Huruma na Masispaa ya Moshi (kitengo cha Damu Salama). Zaidi ya watu 1000 wakiwemo wanafunzi walipima afya na kupata ushauri mbalimbali na watu 50 walichangia damu itakayookoa maisha ya watu 150.

Sr Clementina aliendelea kusema kuwa mbali na zoezi hilo, pia tayari uongozi wa shule hiyo umeshafanya matukio mengine ikiwemo uzinduzi wa maadhimisho hayo ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo na ugawaji wa miti 2,000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambayo itapandwa maeneo mbalimbali mkoani humo.

“Mbali na shughuli hizo, pia zitafuata shughuli zingine ambazo ni pamoja na mbio/matembezi ya hisani km 10 na km 5 zitakayofanyika Agosti 26, 2023 na ambazo usajili wake umeanza leo, (July 7)”, alisema.

Shughuli zote za kuelekea Jubilee ya miaka 25 ya St Mary Goreti zinaratibiwa na kampuni ya Executive Solutions Ltd, Moja makampuni yanayoongoza Nchini katika kuratibu matukio na masuala ya habari.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya St Mary Goreti, Sista Clementina Kachweka akizungumza wakati wa zoezi la upimaji afya na kuchangia damu katika viwanja vya shule hiyo.
Mbunge wa Moshi Mjini, ⁷Priscus Tarimo (kulia) akijiandikisha kushiriki katika mbio/matembezi ya hisani ya Shule ya St Mary Goreti iliyopo Moshi ili kuchangisha fedha za kuwezesha ukarabati wa maeneo mbalimbali wa shule hiyo kama maandalizi ya jubilee ya miaka 25 ya shule hiyo huku Mwalimu Mkuu wa shule hiyo sista Clementina Kachweka (kushoto) akishuhudia. Zoezi hilo la uandikishaji lilienda sambamba na upimaji wa afya na uchangiaji damu.
Mbunge wa Moshi Mjini, Priscus Tarimo akizungumza na wanafunzi zaidi ya 1000 na wageni waalikwa wakati wa hafla ya upimaji afya na kuchangia damu katika viwanja vya St Mary Goreti iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro
Wanafunzi wa shule ya St Mary Goreti wkaifuatilia matukio ya zoezi la upimaji afya na kuchangia damu katika viwanja vya shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad