HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 18, 2023

NBAA TUPO MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM

 



Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) inashiriki maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yenye kauli mbiu "Kukuza ujuzi nchini kupitia elimu ya juu, Sayansi na Teknolojia kwa Uchumi imara na Shindani"

Maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 17 hadi Julai 22, 2023.

Baadhi ya huduma zinazotolewa na NBAA katika kipindi hiki cha maonesho ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)  ni Usajili wa Wanafunzi ili kuweza kufanya mitihani ya Bodi kwa ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya chini (Accounting Technician) mpaka ile ya Taaluma (Profession) pamoja na usajili wa wanachama na makampuni ya Kihasibu na Kikaguzi.

Wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye Banda la Bodi hiyo katika maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yaliyoanza katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Afisa Msaidizi Idara ya Elimu na Mafunzo, Joachim Luguzye (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Abdalmalick Mjuge (kulia) kuhusu namna mwanafunzi anavyoweza kufanya Usajili kwa njia kwenye banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) katika maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Afisa Masoko na Mawasiliano kutoka NBAA Magreth Kageya akitoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) katika maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Afisa TEHAMA kutoka NBAA, Hassan Kawambwa (wa kwanza kulia) pamoja na Afisa Msaidizi Idara ya Elimu na Mafunzo NBAA, Joachim Luguzye wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi walipotembelea Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) katika maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia.
Mzee Omary Kuppa akisaini kitabu cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) mara baada ya kupata elimu kuhusu kazi zinazofanywa na bodi hiyo kutoka kwa Afisa kutoka NBAA Susan Bundala (kushoto) katika maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Afisa Msaidizi Idara ya Elimu na Mafunzo, Joachim Luguzye (kushoto) akitoa elimu kwa Abdalah Mawimbi na Emmanuel Haule kuhusu namna wanafunzi wanavyofanya mitihani ya Bodi katika banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) katika maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Afisa TEHAMA kutoka NBAA, Hassan Kawambwa (kulia) akitoa maelezo kwa Given Maira kuhusu gharama zinazotelolewa na Bodi hiyo wakati wa kufanya mitihani katika banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) katika maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yaliyoanza katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Afisa Msaidizi Idara ya Elimu na Mafunzo, Joachim Luguzye (kushoto) akitoa elimu kwa Israa Khalfan na Sitty Maggid kuhusu namna ya kufanya mitihani ya Bodi katika banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) katika maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yaliyoanza katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam.
Maonesho yakiendelea ndani ya Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambapo Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) wakiwa miongoni mwa washiriki wakitoa elimu katika maonesho hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad