HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 11, 2023

Mkazi wa Kigamboni aipongeza serikali ya Wilaya kuingilia kati mgogoro wa ardhi

 

Mkazi wa Kigamboni Pius Madulu akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la ardhi alilotaka kudhulumiwa  , Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya eneo la hekari 28.5 alilotaka kudhulumiwa Pius Madulu na kusaidiwa na Wilaya ya Kigamboni.

*Madulu kuendelea kuiamini Serikali dhidi watu wanaopokonya ardhi vielelezo vya uongo na kuwabambikia kesi

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mkazi wa Kigamboni Madulu Pius ameipongeza serikali ya wilaya ya Kigamboni kwa kumsaidia kutodhulumiwa eneo lake la ardhi la Hekari 28.5.

Akizungumza na Michuzi TV katika eneo lake Madulu alisema kuwa hadi Serikali ya Wilaya ya Kigamboni kumkabidhi eneo lake alikuwa katika wakati mgumu kutokana na tajiri aliyetaka kumdhulumu kutumia kila njia haramu ya kuchukua eneo hilo.

Amesema Tajiri huyo aliyetaka kumdhulumu alitumia kila hila ikiwemo kutaka kufunga kifungo cha maisha lakini jambo hilo halikufanikiwa.

Madulu amesema kuwa katika maisha yake yalikuwa anaishi kama ndege hadi nyumba yake alifikia kuiogopa kulala akihisi itakuja kuchomwa na huyo mdhulumaji.

Aidha amesema kuwa huyo mdhulumaji wa maeneno ya kigamboni ameshadhulumu watu wengi ambao waliingizwa woga na hawakutaka kufatilia ardhi yao katika serika ya wilaya.

Madulu amesema kuwa akiwa Mkuu wa Wilaya Fatuma Almas Nyangasa mwaka 2022 ndio alifanya maisha yake kuwa na amani ya kurudisha eneo katika mikono yake.

Hata hivyo mdhulumaji alikwenda mbali hata kusema mtu aliyekuwa na eneo hilo amefariki yaani Madulu, na ndiye yeye aliyenunua ardhi ya ndugu Madulu

Madulu amesema sasa anafanya jitihada za kukutana na Mkuu wa Wilaya wa Sasa kumueleza jambo lake ili asitokee dhulumati wa maeneo ya kigamboni kuanza kutengeneza tena migogoro ya kuchukua ardhi kimabamvu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad