Na Mwandishi Wetu,Kigoma
MAKAMU
wa Rais Dk. Philip Mpango, amesema juhudi za kulinda mazingira
zinazofanywa na taasisi mbalimbali kuhamasisha nishati safi ya kupikia
zinastahili kuungwa mkono.
Pia, ameipongeza Kampuni ya Oryx Gas
Tanzania Limited (OGTL) kwa kazi nzuri inayoifanya kuiwezesha jamii
kupata gesi safi ya kupikia kwa kugawa mitungi ya gesi na majiko yake
kwa wananchi, hivyo kutekeleza mkakati wa kuhamasisha matumizi ya
nishati safi ya kupikia.
Dk. Mpango alisema hayo kwa wananchi wa
Wilaya ya Buhigwe, mkoani Kigoma katika hafla ya kukabidhiwa kwa vifaa
mbalimbali kwa wanawake wajawazito ikiwemo mitungi ya gesi 300
iliyokabidhiwa kwa wajawazito 214 na watumishi wa afya ngazi ya jamii 86
kutoka wilaya hiyo.
Mitungi hiyo imetolewa na OGTL kwa
kushirikiana na Taasisi ya Doris Molleli Foundation kwa lengo la
kuwajengea wanufaika mazingira salama ya kupikia na kunusuru uharibifu
wa mazingira unatokana na ukataji miti inayotumika kutengeneza mkaa na
kuni kama nishati ya kupikia.
Akizungumza zaidi wakati akikabidhi
vifaa hivyo pamoja na mitungi ya gesi ya Oryx , Dk.Mpango pamoja na
mambo mengine ametumia nafasi hiyo kuipongeza Oryx Gas kwa uamuzi wa
kugawa mitungi hiyo bura kwa wananchi wa Buhigwe.
"Niipongeze
kampuni ya Oryx Gas kwa kazi nzuri inayoifanya kwa kuiwezesha jamii
kupata gesi safi ya kupikia na hatua hii inastahili kuungwa mkono kwani
inalenga kuendeleza harakati za kutunza mazingira, " amesema Dk.Mpango.
Aidha
Dk.Mpango amewahimiza wanachi wa Buhigwe kutumia gesi ya Oryx kwa kuwa
kampuni hiyo inasaidia jamii kwa kutoa bure mitungi na majiko.
Kwa
upande wake Meneja Mkuu wa Oryx Gas Kanda ya Kaskazini, Alex John,
amesema kampuni hiyo ikiwa kinara wa soko katika usambazaji wa gesi ya
kupikia nyumbani (LPG) nchini, inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa kwa
wananchi kuunga mkono juhudi za serikali za kuhimiza matumizi ya nishati
hiyo.
Ameongeza gesi safi ya LPG ni suluhisho la kutokomeza
matumizi ya kuni na mkaa, hivyo kuboresha afya ya jamii, ustawi na
utunzaji wa mazingira, pia ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk. Samia
Suluhu Hassan la kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia kama
mkakati wa kulinda mazingira.
Amefafanua kwamba kabla ya ugawaji
wa majiko na mitungi hiyo, yalitolewa mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya
gesi yaliyowezeshwa na meneja mkuu huyo wa kanda ya kaskazini.
“Tunaamini
wahudumu wa afya wa wilayani Buhigwe wanawakilisha watu wengi na
wanapaswa kuwa mfano wa mabadiliko ya nishati safi.Sote tunajua kuwa
kundi hili lina ushawishi mkubwa kwa watu wanaowahudumia, hivyo Oryx
tumeamua kutoa mitungi hiyo na majiko ya gesi ya LPG kuwahimiza na
kuwashawishi wengine kuhusu umuhimu wa mabadiliko ya nishati ya LPG,”
amesema.
Pamoja na hayo amesema kampuni ya Oryx Gas Tanzania
inaendelea kuwekeza katika uingizaji, uhifadhi, ujazaji wa gesi kwenye
mitungi na usambazaji wa LPG Tanzania nzima, vikiwemo Visiwa vya Unguja
na Pemba huku akisisitiza kila mwaka kampuni hiyo inatumia mamilioni
kadhaa ya dola katika mitungi mipya inayoletwa sokoni kila siku.
Amesema
kampuni pia inatoa mitungi hii kwa punguzo kubwa, kutoa ruzuku ya
gharama nyingi za LPG kwa vifaa vya kuanzia (Mitungi, Gesi na majiko)
ili kuwawezesha watu kubadili nishati ya kuni na mkaa kwa kutumia gesi
safi na kufanya gesi ipatikane nchi nzima.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation Doris Mollel (kushoto) akizungumza mbele ya Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango(katikati) kabla ya kukabidhi mitungi ya gesi ya Oryx ambayo imegawiwa bure kwa wanawake wajawazito pamoja na wahudumu wa sekta ya afya.Kulia ni wawakilishi wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania.
No comments:
Post a Comment