JAJI MKUU AIFARIJI FAMILIA YA ALIYEKUWA JAJI MKUU WA KWANZA MTANZANIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 24, 2023

JAJI MKUU AIFARIJI FAMILIA YA ALIYEKUWA JAJI MKUU WA KWANZA MTANZANIA

 JAJI Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 24 Julai, 2023 ameitembelea familia aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kwa ajili ya kuipa pole kufuatia kifo cha mama yao mzazi, Bi. Elizabeth Augustine Saidi.


Bi. Elizabeth Agustine Saidi alifariki dunia tarehe 21Julai, 2023 jijini Dar es Salaam.

Mhe. Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma aliitembelea familia hiyo nyumbani kwa marehemu Msasani Mikoroshini jijini Dar es Salaam na kuwapa pole ndugu ,jamaa na marafiki.

Akizungumzia kuhusu msiba huo, mtoto wa marehemu, Bw. Daniel Saidi amesema misa na heshima za mwisho za kumwuaga mama yake zitafanyika siku ya Jumatano, tarehe 26, Julai2023 katika Kanisa la Katoliki la Parokia ya Mtakatifu Petro (St. Peters), Osterbay, kuanzia saa 6 mchana hadi saa 9 alasiri . Kisha mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Marangu Moshi kwa mazishi.

Mazishi ya mama Elizabeth Augustine Saidi yatafanyika siku ya Alahamisi tarehe 27 Julai, 2023 saa saba mchana nyumbani kwake Nduweni Marangu, Moshi.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwapa pole wadogo wa mke wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kufuatia kifo cha dada yao Bi. Elizabeth Augustine Saidi, mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Msasani Mikoroshini jijini Dar es Salaam.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimpa pole Jenerali Mstaafu, Fara Mohamed ambaye ni mjomba wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kufuatia kifo cha Bi. Elizabeth Augustine Saidi, mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Msasani Mikoroshini jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimpa pole Bw. Daniel Saidi ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kufuatia kifo cha mama yake mzazi, Bi. Elizabeth Augustine Saidi, mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Msasani Mikoroshini leo tarehe 24 Julai, 2023 jijini Dar es Salaam.Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika msiba huo.Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na familia ya aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kufuatia kifo cha mama yao, Bi. Elizabeth Augustine Saidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad