IJA YASHIRIKI MAONESHO YA 47 YA KIMATAIFA YA SABASABA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 1, 2023

IJA YASHIRIKI MAONESHO YA 47 YA KIMATAIFA YA SABASABA

 
CHUO cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kinashiriki katika maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika katika viwanja va sabasaba vilivyopo katika Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa kuanzia tarehe 28 Juni, 2023 na yatafanyika mpaka tarehe 13 Julai, 2023 na anategemewa kuzinduliwa tarehe 5 Julai, 2023.

Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto katika maonesho haya kimewakilishwa na Maafisa watatu ambao ni Mhadhiri Ndugu Archibald Kiwango, Afisa Mitihani Bi Dorice Steven na Afisa Uhusiano Bi. Rosena Suka. Banda la Chuo lipo ndani ya Banda kubwa la Mahakama ya Tanzania ambalo lipo barabara ya Sabasaba (Sabasaba Avenue).

Maafisa hawa katika maonesho hayo wanawakilisha Chuo kwa kutoa huduma mbalimbali kama vile kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chuo sambamba na hilo Maafisa hao wanatoa taarifa mbalimbali za wananchi wanaopita bandani za kuwafahamisha sifa za kujiunga na Chuo, Gharama za mafunzo ya muda mrefu na mfupi na kugawa machapisho mbalimbali yanayoandaliwa na Chuo.

Chuo kinatumia fursa ya maonesho haya kuwaalika wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mikoa ya jirani hususani wale wote wenye lengo la kufanya kazi kwenye sekta za utoaji haki Tanzania kuja kutembelea Banda la Chuo ili kupata elimu. Pia kwa wale wote wanatarajia kuwa Madali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama mafunzo mafunzo yataanza tarehe 11 Septermba, 2023. Chuo kinapenda kuwafahamisha wananchi kutembelea kwenye tovuti na mitandao ya kijamii ya Chuo kwa taarifa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad