Kampuni ya Gf Trucks & Equipment’s Ltd ya jijini Dar es Salam imeibuka mshindi wa kwanza katika uuzaji wa Mitambo, Magari ya mizigo vipuli.
Hayo yamebainika wakati wa kuhitimisha Maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es salaam maarufu kama Sabasaba.
Maonyesho hayo yalifunguliwa na Waziri mkuu Kassimu Majaliwa na kuhitimishwa leo na Rais wa Zazibar Hussen Mwinyi na kutoa vikombe na tuzo kwa makampuni mbali mabali yaliofanya vizuri katika Nyanja mbali mbali
Kampuni ya Gf inayojishungulisha na uuzaji wa Magari ya FAW,HONG YANG (trucks) pamoja na mitambo ya XCMG maalumu kwa shuguli za migodini na Wakandarasi wa Barabara.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa Ushindi wa jumla kwa uuzaji wa mitambo na magari(truck) Mkurugenzi wa Masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks ,Salman Karmali alisema wao Ushindi umekuja wakati ambao mradi wa bomba la mafuta unakuja nchin na wao wanaichukulia kama fursa ya kuongeza bidii kwa kuwa karibu na wateja
Pia umoja na mshikamano walionao kati ya wafanyakazi na viongozi ndio chachu ya ushindi huo na pia anawashukluru wafanyakazi woote wa idala mbali mbali kwa kuhakikisha wanafanikiwa pamoja
Mwisho Karmal alisema kampuni hiyo inauza magari ya kisasa ya mizigo aina ya FAW na HONG YANG yanayotengenezwa katika kiwanda kilichopo nchini mkoani Pwani na huraisisha upatikanaji wa haraka kwa mteja ukizingatia sasa hivi mzigo unapatikana hapa hapa na kwa ubora wa viwango vya kimataifa.
Wafanyakazi wa GF wakiangalia gari ya HONG YANG inayotengenezwa na kampuni hiyo katika kiwanda cha Kibaha mkoani Pwani
Wananch waliotembelea maonyesho ya sabasaba wakiangalia gari aina ya FAW
Mtambo wa kutengeneza barabar wa XCMG
No comments:
Post a Comment