HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 7, 2023

DC MATINYI AMEWAASA WAJASIRIAMALI KUPANDISHA THAMANI YA BIDHAA ZAO

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mobhare Matinyi  akiangalia bidhaa mojawapo ya wajasiriamali ambayo  imesindikwa katika moja  ya banda kwenye maonesho  ya Biashara  Kimataifa  yaliyofikia kileke leo Mkoani Dar es Salaam.
DC Matinyi  akiwa katika pichaya pamoja  na walinufaika na mikopo ya 10% ambayo imewawezesha kukuza biashara zao.
DC Mobhare Matinyi  akiangalia kitenge aina ya Batiki.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke  Mobhare Matinyi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika Banda la Manispaa ya  Temeke leo.

Na Khadija Kalili 
MKUU wa Wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi amewashauri wajasiriamali waliowezeshwa kwa kupata mikopo ya asilimia 10 kuboresha bidhaa zao ili ziweze kuleta ushindani katika Soko la Kimataifa.

Ameyasema hayo leo Julai 07, 2023  wakati wa kutembelea Banda la Manispaa ya Temeke katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa  yanayioendelea kufanyika katika viwanja vya SabaSaba jijini Dar es Salaam. Ametembelea na kukagua huduma mbalimbali zinazotolewa na banda la Manispaa ya Temeke.

"Nimefurahi kuona vikundi hivi vya wajasiriamali wakiwa na bidhaa zao, lakini changamoto kubwa si kwa vikundi hivi tu vya Temeke bali kwa nchi nzima kuweza kuboresha bidhaa zao kwa ajili ya kuzipandisha thamani na kuweza kuketa ushindani wa Soko la ndani na nje ya nchi....tuna soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki tunaweza kuuza bidhaa zetu huko katika nchi zaidi ya sita." Amesema DC Matinyi

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Wilaya aezungumzia kuhusu suala la uvamizi wa maeneo ya wazi na kuitaka Idara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuweka matangazo katika maeneo hayo ili kuepuka watu kuyavamia.

Maonesho ya Biashara Kimataifa (SabaSaba) yameanza rasmi Juni 28 mwaka huu na yanatarajiwa kufungwa Julai 13,2023 ambapo Manispaa ya Temeke inashiriki Maonesho haya kwa kusogeza huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo huduma za utoaji wa leseni mbalimbali, huduma za Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa(ICHF) na nyinginezo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad