TANZANIA KUFUNGUA RASMI OFISI ZA UBALOZI INDONESIA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 22, 2023

TANZANIA KUFUNGUA RASMI OFISI ZA UBALOZI INDONESIA

 WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amewasili Jakarta nchini Indonesia kwa ajili ya ziara ya kikazi, ikiwa ni pamoja na kufungua rasmi Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini humo hapo Tarehe 22 Juni, 2023.


Mhe. Dkt. Tax baada ya kuwasili Jakarta amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Mhe. Macocha Tembele katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno-Hatta (CGK).

Akiwa nchini Indonesia Mhe. Dkt. Tax anatarajia pia kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia, Mhe. Retno Marsudi, na kutembelea Chuo cha Diplomasia cha Indonesia.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad