MUSO WANOLEWA, WAASWA KUFUATA MIONGOZO YA CHUO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 12, 2023

MUSO WANOLEWA, WAASWA KUFUATA MIONGOZO YA CHUO

Kaimu RASI wa ndaki Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe na Mhadhiri mwandamizi wa masomo ya uchumi, Dkt. Coletha Komba akizungumza na mwandishi wa habari mara baada ya kufungua mafunzo ya Utawala bora kwa viongozi wa serikali ya wanafunzi. 


Mshauri wa wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe, Mariam Mattao (DSS) akizungumza na Viongozi wa serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es Salaam.

VIONGOZI wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam (MUSO) wameaswa kufanya kazi kwa kadri miongozo ya Serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu Mzumbe.

Hayo yamesemwa na Kaimu RASI wa ndaki Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe na Mhadhiri mwandamizi wa masomo ya uchumi, Dkt. Coletha Komba wakati akifungua mafunzo ya Utawala Bora kwa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi leo Juni 10,2023. Amesema kuwawafuate kanuni na taratibu ili waweze kuendana na matakwa ya serikali yao na chuo kwa Ujumla.

Amesema kuwa nafasi walizozipata wasizichukulie poa kwani ni nafasi kubwa na nzuri za kuongoza na kujifunza kwaajili ya kuongoza sehemu kubwa hapo baadae watakapopata nafasi.

"Tendeni kazi kwa kadri miongozo ya Serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu Mzumbe kwani taratibu na kanuni na taratibu ili waweze kuendana na matakwa ya serikali yao na chuo kwa Ujumla." Amesema

Ametoa wito kwa MUSO kutekeleza majukumu yao kwa wanafunzi wenzao na kukumbuka kuwa bado wanajukumu la kusoma chuoni hapo hata kama wanawaongoza wanafunzi wenzao kwa kila kitu wanachokifanya wafuate mhimili wao kama wanafunzi.

Pia amewaasa wanapoongoza serikali yao wafanye mambo chuo na kuepusha migongano isiyokuwa na maslahi kwao kama wanafunzi ili waweza kuhitimu masomo yao kwa uwingi kama walivyodahiliwa.

Amesema wakufunzi chuoni hapo wanafundisha kwa kupitia misingi ambayo imewekwa kwaajili ya kuendeleza wanafunzi kitaaluma na kijamii hivyo wanafunzi hata wakihitimu chuoni hapo watakuwa vizuri kwa sababu wamepita kwenye mikono salama ya mafunzo.

"Uwe kiongozi, usiwe kiongozi lakini kwa kila jukumu ambalo utapewa ulifanye basi utalifanya kwa misingi ambayo umefundishwa chuoni na kuleta matokeo mazuri zaidi." Amesema

Mafunzo hayo yametolewa kwa Viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa wa serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe.

Kwa Upande wa Mkufunzi wa masuala ya usimamiaji wa Fedha kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Erasto Silayo amesema amewaasa viongozi hao kuwa na uwazi katika matumizi ya mapato ya serikali ya wanafunzi Chuoni hapo.

Mafunzo hayo yamehusisha namna ya kuongoza vikao, kukasimisha madaraka, usimamizi wa fedha, Masuala ya Mawasiliano pamoja na Miiko yake na jinsi ya kutatua migogoro.
Mkufunzi wa Masuala ya ubora wa viongozi, Dkt. Lusekelo Kasongwa akitoa elimu kwa viongozi waSerikali ya wanafunzi Mafunzo yaliyofanyika ndaki ya Dar es Salaam.Mkufunzi wa mawasiliano kutoka Chuo Kikuu Huria, Sophia Mchimbi akizungumza na viongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam. 


Baadhi ya Viongozi wa Serikali ya wanafunzi wa chuo Kikuu Mzumbe, ndaki ya Dar es Salaam wakichangia maada wakati wa mafunzo ya utawala bora yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa masuala ya usimamiaji wa Fedha kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Erasto Silayo akitoa mada kwa viongozi wa serikali ya wanafunzi.
Picha ya pamoja.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad