KONGAMANO LA 26 LA MCT LAFUNGULIWA JIJINI DAR, KAMISHNA WA ELIMU AMEOMBA SERIKALI KUWEKEZA KATIKA ELIMU YA AWALI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 12, 2023

KONGAMANO LA 26 LA MCT LAFUNGULIWA JIJINI DAR, KAMISHNA WA ELIMU AMEOMBA SERIKALI KUWEKEZA KATIKA ELIMU YA AWALI


Kamishna wa elimu nchini Lyabwene Mutahabwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 12, 2023 mara baada ya kufungua kongamano la 26.KAMISHNA wa elimu nchini Lyabwene Mutahabwa ameiomba Serikali kuongeza jitihada zaidi katika kuwekeza kwenye elimu ya awali kwa sababu elimu hiyo ndiyo msingi wa kumjenga mtoto kukua kiakili na fikra.

Hayo ameyasema wakati wa  kufungua kongamano la 26 lililoandaliwa na Chama cha Montesori Community of Tanzania (MCT) jijini Dar es Salaam leo Juni 12, 2023 ambalo linajadili njia za ufundishaji kwa kutumia njia ya Montessori. Amesema njia hiyo inaweza kuwa msaada mkubwa kwa ujenzi wa watoto wa kitanzania wenye muelekeo mpana na kuhoji mambo mbalimbali katika jamii.

Ameongeza Montessori itasaidia pia wazazi kutambua uwezo wa watoto wao na itawasaidia pia kuwafanya wazazi na watoto kuwa karibu.

"Tukizubaa kuwekeza kwenye ngazi hii ya awali taifa limekwisha hivyo nimewaelekeza wapige jaramba usiku na mchana kwenye vyombo vyote tuwekeze iwezekanavyo katika malezi na makuzi na maendeleo ya awali ya watoto wetu." Amesema Mutahabwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa MCT, Sarah Kiteleja amesema ufundishaji kwa njia ya Montessori amesema ni mbinu pekee inayomuandaa mtoto kuwa mwenye kujiamini ili anapokuwa mkubwa anakuwa na uelewa na kuwa katika hali anayoipenda.


"Tunamjenga mtoto mwenye ujasiri na uthubutu lazima tumjengee msingi na muendelezo na kile alichowekewa na Mungu na kumpata yule tunayetaka kuwa, hivyo sisi Montessori tumewekeza zaidi kwa watoto wadogo kwa sababu tunaamini  tukiwapa mazingira na nafasi ya wao kujijengea kujiamini ili anapokuwa mkubwa aweze kufanya masomo yake kwakujiamini," amesema Kiteleja.

Naye Mwenyekiti wa MCT, Martha Dello amesema malengo ya kongamano hilo kila mwaka huwa ni kuwakutanisha wazazi na walezi kwa pamoja ili waweze kukumbushana na kupeana mambo mapya katika kumlea na kumkuza mtoto vizuri.

Licha ya hayo wazazi na walezi nchini wametakiwa kuwakuza  watoto kwa misingi imara ya kimwili na akili kutengeneza Taifa bora.

Awali  Mgeni rasmi amewataka wazazi na walezi kutokuwaachia walimu pekee katika elimu ya awali na msingi ambayo ndio huanza kumjenga mtoto kiakili na Mwili.

Aidha amewaasa  wazazi kuwa licha ya kuwapeleka shule watoto kupata elimu pia wawape  wasaha Wa kujifunza maisha halisi ya kitanzania yatakayo wasaidia watoto uwelewa Wa kutosha kuhusu Jamii yao kuweza kukabiliana na  changamoto mbalimbali zilizopo nchini.

Hata hivyo katika kongamano hilo Mkurugenzi Mtendaji Wa Montessori  Sarah Kiteleja amesema lengo la kongamano hilo ambalo hufanyika kila  mwaka  ni kuwajengea uwezo walezi wa vituo vya watoto na walimu,kukumbushana na kutathimini nini kifanyike kukuza watoto katika misingi iliyo imara ya tabia na akili ili kuwajengea watoto uwezo kuchanganua maswala mbalimbali.
Kamishna wa elimu nchini Lyabwene Mutahabwa akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 26 lililoandaliwa na Chama cha Montesori Community of Tanzania (MCT) ambalo linajadili njia za ufundishaji kwa kutumia njia ya Montessori.


Baadhi ya washiriki wa Kongamano la 26 lililoandaliwa na Chama cha Montesori Community of Tanzania (MCT) ambalo linajadili njia za ufundishaji kwa kutumia njia ya Montessori wakiwa katika kongamano hilo litakalofanyika kwa siku tano.
Picha za pamoja za baadhi ya washiriki  wa Kongamano la 26 lililoandaliwa na Chama cha Montesori Community of Tanzania (MCT) ambalo linajadili njia za ufundishaji kwa kutumia njia ya Montessori.
Mwenyekiti wa MCT, Martha Dello akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kongamano la 26 linaloendelea kufanyika katika Ukumbi wa Msimbazi Centre.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa MCT, Sarah Kiteleja akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 12, 2023 mara baada ya kufungua kongamano la 26.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa MCT, Sarah Kiteleja akifafanua jambo kwa Kamishna wa elimu nchini Lyabwene Mutahabwa alipotembelea moja ya darasa ambalo linambinu zote za kufundishia.

Matukio mbalimbali wakati wa kongamano la 26 la Chama cha Montesori Community of Tanzania (MCT).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad