HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 1, 2023

CBE yaja na kozi mpya 16 zikiwemo za ujasiriamali na uvumbuzi

 · Lengo ni kuwawezesha vijana kupata ajira za chap chap wanapohitimu


Na Mwandishi Wetu
CHUO  cha Elimu ya Biashara (CBE) kuanzia mwaka wa masomo wa 2023/2024 kimepanga kuwapa wanafunzi ujuzi na maarifa muhimu katika fani za ujasiriamali, Uvumbuzi, Uchumi, Fedha, Usafirishaji, Usimamizi wa Vifaa na Masoko kidigitali zinazokwenda na soko la ajira.

Hayo yalisemwa jana na Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Tandi Lwoga, wakati akizungumza na waandishi wa habari kutambulisha kozi mpya katika taasisi yetu ambazo zitaanza kutolewa katika mwaka wa masomo utakaoanza Oktoba 2023.

Alisema prgramu hizo mpya zitajumuisha kozi za vyeti vya ufundi wa Msingi Vyeti vya Ufundi, Shahada za kwanza, na Shahada za Uzamili.

Profesa Lwoga alisema CBE inajivunia kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya Biashara ya hali ya juu kwa miaka 58 sasa, inayokidhi mahitaji ya soko la ajira na kukuza ujasiriamali nchini.

Alisema kozi hizo ni matokeo ya tafiti za kina na jitihada za muda mrefu zilizofanywa na timu yetu ya wahadhiri pamoja na wadau mbalimbali waliobobea katika tasnia husika na zimezingatia mabadiliko ya teknolojia inayokua kwa kasi, mazingira ya uwekezaji, viwanda na biashara, na mahitaji ya soko la ajira.

Alisema kozi hizo zinakusudia kutoa ujuzi wa vitendo, maarifa ya hali ya juu, na mafunzo ya kina kwa wanafunzi wa chuo hicho ili kuwawezesha kufanikiwa katika soko la ajira na kukabiliana na changamoto za wakati wetu.

Ninaomba sasa nizitaje kozi Mpya kama ifuatavyo;-

Alitaja kozi hizo kuwa ni za za Vyeti vya ufundi wa Msingi ambazo zitajumuisha, ujasiriamali na ubunifu, uchumi na fedha, usafirishaji na utafutaji masoko kidijitali.

Alisema chuo pia kitatoa Shahada za Kwanza katika kozi za ujasiriamali na ubunifu, usafirishaji, uchumi na fedha na Shahada za Uzamili kwenye Usimamizi wa Miradi Tathmini na Usimamizi .

Alisema kupitia Mradi maendeleo endelevu kiuchumi (BUSEDA), CBE itaanza kutoa mtandaoni au kozi ya kuptia mtandao kwa wanafunzi wote wa Shahada za Uzamili ambayo itawapa ujuzi maalum kuhusu fursa za uwekezaji na biashara kwa ajili maendeleo ya kiuchumi katika nchi washiriki ambazo ni Finland pamoja na nchi tano za Africa, ambazo ni Mauritius, Sheli Sheli, Malawi, Lesotho na Botswana.

Alisema kozi hiyo inafadhiliwa na taasisi iitwayo Team Finland Knowledge Programme ambayo ipo chini ya Finnish National Agency for Education nchini Finland.

Alitaja taasisi zinazoshiriki kuwa ni Chuo Kikuu cha Mashariki mwa Finland (Mshirika Mkuu), Chuo Kikuu Huria cha Botswana, Chuo Kikuu cha Taifa cha Lesotho, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Tanzania, Chuo Kikuu cha Malawi, Chuo Kikuu cha Mouritius na Chuo Kikuu cha Sheli Sheli.

“Kozi hii inalenga kukuza uhusiano wa kibiashara, ujasiriamali, na uwekezaji kati ya Afrika na Finland na itatolewa kwa wanafunzi wote wa Shahada ya Uzamili kupitia mtandanoni ikiwa ni mara ya kwanza mwezi Oktoba 2023,” alisema.

Profesa Lwoga alisema wanafunzi wataweza kujifunza fursa mbalimbali za kibiashara na jinsi ya kuwekeza Tanzania pamoja na nchi hizi tano za Africa, na Ulaya (Finland) zilizopo ndani ya mradi wa BUSEDA na kwamba ingawa yatatolewa mtandaoni lakini wanafunzi watajifunza kwa vitendo.

Alisema kuzinduliwa kwa kozi hizo mpya ni hatua muhimu katika kuongeza ubora wa elimu inayotolewa na Chuo hicho na kwamba wanaamini kuwa programu hizo zitawawezesha wanafunzi wao kuwa na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira la leo na kujenga msingi imara wa ujasiriamali.

“Mchakato wa maombi unaanza leo na wanafunzi wote wanaotaka kujiunga na kozi za Astashahada, Stashahada na Shahada za Uzamili. Mchakato wa maombi kwa Shahada za Kwanza tutawatangazia na waombaji ninawaomba kutembelea tovuti ya CBE www.cbe.ac.tz kwa maelezo zaidi na kufanya mchakato wa maombi,” alisema.
Kaimu Mkuu wa chuo cha elimu ya Biashara (CBE), Profesa Tandi Lwoga, akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo jijini Dar es Salaam kuhusu kuanza kwa kozi mpya 16 kwenye mwaka huu wa masomo wa 2023/2024. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Leonidas Tibanga na kulia ni Mkurugenzi wa Taaluma chuoni hapo. Dk. Shima Dauson.
Kaimu Mkuu wa chuo cha elimu ya Biashara (CBE), Profesa Tandi Lwoga, akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo jijini Dar es Salaam kuhusu kuanza kwa kozi mpya 16 kwenye mwaka huu wa masomo wa 2023/2024. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Leonidas Tibanga na kulia ni Mkurugenzi wa Taaluma chuoni hapo. Dk. Shima Dauson.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad