BRELA WAWAKARIBISHA WAFANYABIASHARA KATIKA MAONESHO YA BARCODE JIJINI DAR - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 16, 2023

BRELA WAWAKARIBISHA WAFANYABIASHARA KATIKA MAONESHO YA BARCODE JIJINI DAR


WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamewakaribisha wananchi na wafanyabiashara katika Maonesho ya Barcode yanayofanyika Viwanja vya Mnazi. Mmoja jijini Dar es Salaam kujipatia huduma zinazotolewa na Wakala hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Juni 16,2023, Msajili Msaidizi kutoka BRELA, Benedikson Willson amesema kuwa wapo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kuwahudumia wananchi, wajasiriamali na wafanyabiashara mbalimbali iliwaweze kuhuisha taarifa za biashara na Kusajili majina ya kampuni na kupata haki kisheria.

Huduma nyingine wanayotoa ni kusajili alama za biashara zitakazo wasaidia kutangaza biashara sokoni. ... "Mteja akija anakuwa anajua bidhaa gani anaenda kununua kulingana na alama ambayo itakuwa imewekwa kwenye bidhaa." Ameeleza Wilson

"Tupo katika Maonesho ya Barcode sisi kama wadau wa biashara na wasajili wa huduma mbalimbali za kibiashara ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kuwahudumia."

Akitolea mfano, Willson ameeleza kuwa mteja hata kama anaenda kukunua nguo ya nembo (Brand) flani kulingana na utambulisho wa bidhaa anayohitaji sokoni.

Aidha ametoa wito kwa wananchi na wafanyabishara mbalimbali kutembelea maonesho hayo ili kujipati huduma zinazotolewa na BRELA.

Amesema kuwa kama Mwananchi anataka jila la biashara unatakiwa kuwa na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) pamoja na Email tuu baada ya hapo utasajiliwa na kuondoka na jina la biashara kabisa.

Huduma wanaozitoa ni pamoja na Kusimamia sheria za usajili wa biashara na kurasimisha biashara, kusajili Makampuni, kusajili majina ya biashara, Kusajili alama za biashara na huduma, kutoa leseni za biashara, kutoa leseni za Viwanda zenye sura za kitaifa na kimataifa na kutoa Ataza.

Kwa wa Mteja wa BRELA, Masanja Mboyi amepongeza wakala hiyo kwa Kutoa elimu katika Maonesho ya Barcode yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja maonesho yanayokusanya wanchi wa kada mbalimbali.

"Huduma wanazotoa hapa ni zuri, na Wananchi wanakipata kile wanatarajia na kile ambacho hakitarajiwi kulingana na maswali ya mteja mwenyewe nini anataka kijua."

Amesema kuwa maonesho hayo yamekuwa ya mda mfupi, angetamani yangefanyika kwa wiki nzima lakini yanaisha jumatatu, Juni 19,2023 pamoja na kutoa elimu kwa muda huo ameelimika.

Huduma za BRELA ni nzuri kwani zinatolewa kisasa zaidi, unaweza kupata huduma ana kwa ana pia unapata huduma kieletroniki mfano kuprintiwa Nyaraka, unachotaka kukiona kupitia mitandao, kwa vitu visivyo kieletroniki tunapata maelezo kwa kina." Amesema Mboyi

Msajili Msaidizi kutoka BRELA, Benedikson Willson kizungumza jijini Dar es Salaam leo  Juni 16, 2023 katika Maonesho ya Barcode yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya maafisa kutoka BRELA wakiwahudumia wananchi waliotembelea katika banda lao lililopo katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Mteja wa BRELA, Masanja Mboyi akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kupata elimu katika banda la BRELA katika maonesho ra Barcode yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad