HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 19, 2023

WANAOLIMA NA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA WAFICHULIWE -SHAIB

 


Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
KIONGOZI wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka huu, Abdallah Shaib amekemea wale ambao wanalima na kusafirisha madawa ya kulevya kwani ndio chanzo kikuu kinachochagiza ongezeko la waraibu wa madawa ya kulevya.


Alitoa rai hiyo Mjini Kibaha Mkoani Pwani baada ya kufika asasi ya Oyarb- Kongowe,kuona shughuli zinazofanywa katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya na kutoa ushuhuda.

Aidha ameiasa,Jamii kuacha kuwanyanyapaa waraibu wa madawa ya kulevya, kwa kuwaita MATEJA, na badala yake wasaidiwe kupata ushauri ili waache tabia hizo.

Alieleza, ili kuhakikisha wanakuwa raia wema wa kitanzania kwa kuachana na uraibu ni vyema kukaa nao,kuwakumbusha athari za madawa hayo.

Shaib alisema kuwa, janga la madawa ya kulevya ni tatizo mtambuka ambalo linaathiri Taifa, Afrika na Dunia.

"Vipo viashiria vya wazi ambavyo vinaonyesha uwepo matumizi ya madawa ya kulevya ambavyo vinaathiri kundi la vijana 13-24 ambao ni nguvu kazi ya Taifa na wanahitaji kupata elimu bora "alielezea Shaib.

Aliitaka jamii kushirikiana na Serikali na Jeshi la polisi kutoa taarifa pale wanapobaini kama kuna mtu ama kundi la watu linajihusisha na shughuli hizo ili vikomeshwe na kuokoa nguvu kazi inayopotea.

Akiwa ofisi ya Oyarb zilizopo Kongowe,kuona shughuli zinazofanywa katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya, Ofisa Maendeleo Joyce anasema , waraibu waliopo katika tiba ya methadone ni 431 kati yao wanaume 228 wanawake watatu na walioacha ni 37.

"Kwanza wanasajiliwa,wanapata ushauri nasaha katika asasi hiyo kisha wanapata rufaa ya tiba ya methadone kwenye hospital ya rufaa Tumbi, Halmashauri imejipanga kutoa tiba kwa waraibu na wanawafuatilia kwa matumizi salama ya tiba ya methadone"alielezea Joyce.

Awali akipokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Halmashauri ya Kibaha Vijijini, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mshamu Munde alieleza,Mwenge huo umepitia miradi 12 yenye thamani ya Tsh.Bilioni 3.9.Miradi hiyo imetekelezwa kwa fedha toka sehemu mbalimbali ambapo Tsh.520,297,499.98 ni mchango wa Halmashauri .


Alieleza ,sh.683,710,900 zimetoka Serikali kuu huku Tsh.2,405,097,550 zikigharamiwa na Wananchi na wahisani wakitumia kiasi cha Tsh.293,350,000.00.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad