HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 10, 2023

WANANCHI CHANGAMKIENI FURSA ZA ZABUNI ZA UMMA

  

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI kupitia Mamlaka ya kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) imewataka wananchi kuchangamkia fursa zinazipatikana katika sheria ya ununzi wa umma ili kuweza kunufaika nazo katika juhudi za kutokomeza umasikini nchini.

Hayo yamesemwa Mei 8 na Meneja Uhusiano kwa Umma PPRA Bi. Zawadi Msalla wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Jijini Dodoma.

Amesema kuwa, licha ya serikali kuwa na mfumo rahisi wa kuweza kufanya biashara na wazabuni kwa kufuata misingi ya haki na sheria lakini jamii imeonekana bado kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya fursa hizo.

“Watu wengi wanaonekana kutokuwa na uelewa juu ya urahisi wa kupata zabuni za serikali, ndio maana baadhi yao wanaishia kulalamikia kwa kudhani kuwa serikali inapendelea upande fulani, jambo ambalo sio kweli” Amesema.

Kupitia mfumo wa ununuzi kwa njia ya mtandao, serikali hutangaza zabuni mbalimbali kwa kuzingatia misingi ya haki , ushindani na uwazi.

Mpaka sasa tangu kuanzishwa mfumo huo ni wazabuni 30,200 pekee ndio waliojisajili katika mfumo huo ili kupata zabuni za serikali . Idadi inayoonekana kuwa ni ndogo zaidi kuliko idadi ya wazabuni waliopo suala linalopelekea kujirudia kwa wazabuni walewale mara kwa mara kila zinapotangazwa zabuni za Serikali.

Akizitaja baadhi ya fursa hizo amesema, zipo fursa zenye ushindani wa kimataifa ambazo huwapa upendeleo zaidi wazabuni wa ndani ya nchi wanaotaka kufanya biashara na serikali kwa kuwapa upendeleo wa asilimia kumi zaidi dhidi ya wageni, huku biashara ya bidhaa za ndani zikipewa upendeleo wa hadi asilimia kumi na tano dhidi ya bidhaa zitokazo nje ya nchi.

Zaidi ya asilimia sabini ya bajeti ya Serikali huenda katika ununuzi. Kwa kuzingatia hilo ni jukumu la PPRA kuhakikisha ununuzi wote unaofanyika iwe ni wa bidhaa, kazi za ujenzi au huduma unazingatia miiko ya ununuzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad