HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 2, 2023

TGNP WATOA MAFUNZO KWA WANAMASOKO, MAWASILIANO YA UMMA NIT JIJINI DAR

 Na Mwandishi wetu.

MTANDAO wa Kijinsia Tanzania (TGNP) wakishirikiana na Internews kupitia Mradi wa Boresha habari watoa mafunzo kwa Wanachuo wanaosoma Kozi ya Masoko na Uhusiano ya Umma katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Akizungumza wakati wa Kutoa Mafunzo hayo, jijini Dar es Salaaam leo, Mei 2, 2023, Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia wanachuo hao katika Masoko na Mahusiano na Umma watakao kiwa wakifanya kazi kwa Mrengo wa na jicho la Kijinsia.

Amesema elimu hiyo inatakiwa kutolewa katika ngazi zote za elimu ili kuondoa na unyanyasaji wa kijinsia unaofanyika katika jamii bila kujua kuwa wanakandamiza jinsi nyingine.

Akizungumzia kuhusiana na Majukumu ya jinsi (Sex) ya 'Me' na' Ke' amesema kuwa majukumu ya jinsi ya 'Ke' ni kubeba Ujauzito na kujifungua pamoja na kunyonyesha huku akizungumzia jinsi 'Me' ni kutungusha mimba na Majuku mengine yote yanaweza kufanywa na jinsi zote.

Amesema kuwa jamii imeshindwa kitofautisha kati ya 'sex' ambayo ni jinsi na 'Gender' ambayo ni Jinsia amesema jinsia inawakilisha majukumu hasa ya mwanamke na Mwanaume.

Akitolea mfano katika picha zilizoambatana na mada hiyo imeonesha mwanamke anaujauzito, amebeba mtoto mgongoni kichwani akiwa na kuni na mkononi akiwa na ndoo ya maji, Temba amesema kuwa katika picha hiyo kitu ambacho mwanaume hawezii kumsaidia mwanamke huyo ni kubeba mimba lakini vitu vingine angeweza kumsaidia na mke wake ila jamii inaona kama majukumu hayo yote ni ya mwanamke.

Pia ameiomba jamii kubadilika na kuungana na wanamke kufanya majukumu yote ya familia isipo kuwa yale ambayo ni ya kibaolojia tuu ambayo yamegawanywa kwa Jinsi Ke na Me ambayo hakuta mmojawapo anayeweza kumsaidia mwenzie isipo kuwa mwenye majukumu yake tuu.

Pia amesema Jamii iungane na Serikali katika kusaidia kumpunguzia amajukumu mwanamke hasa serikali inapo saidia KUMTUA NDOO KICHWANI MWANAMKE kwa kusogeza huduma ya maji ya uhakika karibu na jamii na vile serikali inahamasisha kutumia NISHATI SAFI YA KUPIKIA hiyo inaonesha dhahili jinsi ya kumsaidia mwanamke kuachana na kwenda kukata kuni Porini kwa kutumia muda mwingi kwenda kutafuta kuni badala ya kufanya shughuli za maendeleo.

Aidha amewaomba wanachuo waliopata mafunzo yenye Mrengo wa kijinsia kutekeleza majukumu yao kwa jicho la kijinsia ili kutokomeza kabisa unyanyasaji unaofanywa na jamii na hata katika ngazi ya familia.

Akizungumzia umuhimu wa Utoaji elimu hiyo katika ngazi mbalimbali za jamii Temba amesema kuwa hata walimu katika shule za msingi wanatakiwa kupata elimu hiyo ili wanapotoa majukumu kwa wanafunzi hasa ya kwenda kuchota maji na kukata kuni yawe ya wanafunzi wote sio wasichana tuu.

Akitolea mfano wa picha moja wapo iliyopo kwenye mada hiyo ikionesha mtoto wa kiume akienda shule na mtoto wa kike akienda kutafuta maji, Temba ameeleza kuwa sio kuwa watoto wa kike hawafaulu mitihani kwa kukosa kuelewa bali kwa kuwa na uchovu wa kuchoka wakati wakitimiza majukumu mbalimbali na wanaishia kusinzia wakati watoto wa kiume wakitumia muda huo kujisomea.

Kwa upande wa Mwanachuo wa NIT, Kelvin Brazio amesema kuwa mafunzo hayo yatamsaidia katika kutatua changamoto mbalimbali ambazo zitasaidia kumpunguzia majukumu mwanamke kwa kuwa majukumu mengi kila mmoja anaweza kufanya.

Pia ameiomba serikali kutoa elimu ya Jinsi na Jinsia kwa jamii kubwa zaidi ili kuhakikisha kila jinsi inafanya majukumu yote yaliyopo katika familia kama kupika, kuosha vyombo, kufua pamoja na kuchota maji.

Akizungumzia kuhusiana na Mafunzo hayo Maria Paul ambaye ni Mwanchuo wa NIT, amesema kuwa jamii lazima ibadilishe fikra juu ya majukumu ya familia kwani mafunzo waliyopewa yanaonesha dhahili majukumu mhimu kuwa ni ya kibiolojia tuu na maengine yanawezekana kufanywa na mtu yeyote sio mwanamke tuu kama jamii inavyofikiria.
Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akizungumza wakati wa kutoa elimu ya Kijinsia kwa wanachuo wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) jijini Dar es Salaaam leo, Mei 2, 2023.
Baadhi ya  wanachuo cha NIT wakimsikiliza mwezeshaji kutoka TGNP jijini Dar es Salaaam leo, Mei 2, 2023.

Baadhi ya  wanachuo cha NIT wakichangia mada wakati mwezeshaji kutoka TGNP akitoa mada jijini Dar es Salaaam leo, Mei 2, 2023.









Matukio Mbalimbali.

Picha za pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad