HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 22, 2023

TCAA YAENDELEA KUFANYA VIZURI KATIKA KUIMARISHA USAFIRI WA ANGA NCHINI


Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeendelea kuonesha ufanisi katika anga za kimataifa ambapo Tanzania kupitia Mamlaka hiyo imechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu wa Usafiri wa Anga Barani Afrika (The African Flight Procedure Programme - AFPP) kwa kipindi cha Miaka mitatu (3) kuanzia mwaka 2022/23 – 2024/25. Kazi kubwa ya Kamati hii ni kujadili uendelezaji wa miundombinu ya njia za ndege angani.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Makadirio mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024, Bungeni Jijini Dodoma ambapo amesema Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeendelea kutoa vyeti vya ubora kwa ndege ambapo hadi kufikia Aprili mwaka 2023 jumla ya ndege 16 zilisajiliwa na kufanyiwa ukaguzi na kupewa vyeti vya ubora (Cirtificate of Airworthiness).

"Wizara kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeendelea kutoa huduma za udhibiti wa usafiri wa anga, viwanja vya ndege, masuala ya kiusalama na kiuchumi katika huduma za usafiri wa anga pamoja na kutoa huduma za uongozaji ndege katika viwanja 14 vya Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza, Arusha, Pemba, Tabora, Kigoma, Dodoma, Iringa, Songwe, Mtwara, Tanga, Songea na Kilimanjaro". amesema Prof. Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Makadirio mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024, Bungeni Jijini Dodoma.
Mnara wa kuongozea Ndege wa TCAA uliopo Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
Muongozaji Ndege akiwa Kazini

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad