Nahodha wa Usimamizi wa Majini wa Kituo cha Utafutaji na Uokoaji wa TASAC Alex Katama akionesha umuhimu wa vifaa vya uokozi kwa wavuvi wakati utoaji wa elimu katika moja ya kambi ya Wavuvi wa Kaole Bagamoyo hawapo pichani.
Nahodha wa Usimamizi wa Majini wa Kituo cha Utafutaji na Uokoaji wa TASAC, Alex Katama akizungumza wavuvi wa Kaole Bagamoyo kuhusiana na usalama vyombo vya majini ikiwa ni muendelezo wa TASAC kutoa elimu.
Matukio mbalimbali ya utoaji wa elimu kwa wavuvi katika Kambi Kaole Bagamoyo mkoani Pwani.
*Yawataka wamiliki wa vyombo vidogo vya majini kuwa na vifaa Okozi wakati wa kukabidhi vifaa vya Wavuvi.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema ni lazima vyombo vidogo vya usafiri wa majini kuwa na vifaa okozi na kuvaa jaketi okozi kabla kuanza safari kwenye bahari, maziwa, mito na mabwawa.
Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu kwenye kambi za Wavuvi wa Kaole, Changwahela na Mlingotini wilayani Bagamoyo, Mkaguzi wa vyombo vya usafiri Majini na msimamizi wa Kituo cha Utafutaji na Uokoaji wa TASAC, Nahodha, Alex Katama amesema kuwa vyombo vidogo vya Usafiri Majini, marufuku kuanza safari zao bila kuwa na vifaa vya uokozi, kuto toa taarifa sahihi kwa BMU, serikali za mtaa, au kwa wasimamizi wa fukwe anapotia nanga. Hiyo ni sheria ya usimamizi wa usalama wa usafiri.Nia ni kuokoa maisha ya nguvu kazi za watanzania na kupunguza madhara ya ajali inapotokea chombo kupigwa na wimbi au hali hewa inapobadilika ghafla.
Katama amesema kuwa elimu ambayo wamekuwa wakiitoa TASAC imefanya vifo vinavyotokana na ajali za vyombo vidogo vya usafiri wa maji kwenye bahari na maziwa kupungua. Hayo ni mojawapo ya mafanikio katika utoaji wa elimu.
Nahodha huyo ameeleza kuwa wamiliki wa vyombo vya usafiri majini wanatumia gharama kubwa kutengeneza hivyo vyombo na hakuna sababu ya kutonunua vifaa vya uokozi.
"Wamiliki ambao hawana vifaa vya uokozi kuendelea kufanya kazi kuingia baharini bila vifaa hivyo waache maana wanaweka rehani maisha ya wavuvi na wafanya kazi wao.Pia, wanahatarisha maisha ya watu na kinyume cha sheria"amesema Nahodha Katama.
Amesema kuwa vifaa vya uokozi katika safari za majini ya uvuvi na safari za kawaida huvaliwa kabla ya safari kuanza kutokana na vifaa hivyo kuendelea kuwepo bila kuvaliwa wakati janga linapotokea hakuna hata mmoja anaweza kukumbuka uwepo wa vifaa hivyo na kusababisha madhara makubwa ikiwemo na vifo.
Amesema katika elimu hiyo pia kuwaambia namba ya bure kupiga pale wanapoona madhara yanatokea ikiwemo kupotea."Ukiwa na simu funga kwenye karatasi isiyoingiza maji na kupiga Filimbi wakati wanatafutwa na waokozi alisema Alex.
Afisa Ukaguzi Jeshi la Zimamoto SSGT, Mganga Mkama amesema kuwa wanaotumia vyombo vya moto vinavyotumia mafuta wanatakiwa kuwa na vifaa vya kuzimia moto' Fire extinguisher' au kipande cha blanketi.
Amesema, vyombo vya majini vinatumia mafuta inaweza kuungua kwani moto wa mafuta huweza kuzima kwa kutumia maji kwa sababu maji hujitenga na mafuta na kuendelea kuunguza kwa abiria na manahodha pamoja na mali.
No comments:
Post a Comment