HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 4, 2023

SERIKALI IKO HATUA ZA MWISHO KUKAMILISHA MKAKATI KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO

SERIKALI kupitia Taasisi kama  Wakala wa Majengo (TBA),Shirika la Reli Tanzania (TRC), na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wako hatua za mwisho za kukamilisha mkakati wa namna ya  kushirikiana na sekta binafsi kutekeleza majukumu yao.

Mfano tu ukikamilika mradi wa SGR ,kutakuwa na vipande vitakavyokuwa vikifanyiwa ukarabati na sekta binafsi badala ya TRC wenyewe huku ikielezwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa kipaumbele kwa taasisi binafsi hususani katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa jijini Arusha na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya wakati akifungua mkutano wa tatu wa kikanda wa mashauriano na wadau wa sekta ya ujenzi kwa mwaka 2023 ulioanadaliwa na Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Arusha kwa wadau wa ujenzi wa mikoa ya kanda ya kaskazini.

Aidha imeelezwa makandarasi wa ndani wametakiwa kutumia wataalam wenye sifa katika kutekeleza shughuli zao, ili kuweza kukidhi vigezo hitajika na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kupunguza matumizi ya wakandarasi wa nje hususani katika miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB),Mhandishi Joseph Nyamhanga, ameishukuru Serikali kupuguza matumizi ya force akaunti,hususani katika majenzi hali ambayo imeamsha tena hari ya makandarasi wa ndani kufanya kazi.

Nyamhanga amesema , “Tunashukuru Serikali kwa kuliona hili,force akaunti sio mbaya,kutumia katika ujenzi wa darasa moja katika shule inaruhusiwa,lakini kwa miradi mikubwa tunaomba serikali itumie Makandarasi”.

Wakati huo huo Msajili wa Bodi ya Makanadarisi Mhandisi Rhoben Nkori ametoa mwito kwa makandarasi wa ndani kuandika bei halisi ya miradi yao,wakati wa usajili miradi yao kwa CRB,kwani imebainika baadhi ya makandarasi kuandika gharama ndogo ya miradi yao tofauti na mikataba waliyoingia.

“Tumebaini baadhi ya makandarasi kuandika gharama ndogo ya miradi yao,wakati wa kutembelea shughuli zao tunakuta gharama ya mradi ni tofauti na aliyosajilia mradi kwenye mfumo,hii ni kinyume cha sheria”.amesema Mhandisi Nkori.

Mkutano huo wa siku mbili umewakutanisha makandarasi kutoka mikoa sita ya kaskaskazini na mikoa jirani ,ikiwemo mkoa wa Arusha,Kilimanjaro,Manyara,Tanga,Singida na Dodoma,ambapo makandarasi watajadili na kuweka mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta ya makandarasi nchini.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya.

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi Mhandisi Joseph Nyamhanga.

Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi Mhandisi Rhoben Nkori

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad