JAMII YASHAURIWA KUFUATILIA MIRADI YA MAENDELEO KWENYE MAENEO YAO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 2, 2023

JAMII YASHAURIWA KUFUATILIA MIRADI YA MAENDELEO KWENYE MAENEO YAO

 Njombe

JAMII imetakiwa kutoa taarifa ya kukosekana kwa uwajibikaji katika Utekelezaji wa miradi ya umma katika maeneo yao ili kuzisaidia mamlaka kuchukua hatua mapema na kunusuru ubadhirifu na upotevu wa fedha za walipakodi.

Moja ya sababu inayotajwa kusababisha ubadhirifu katika miradi ya umma ni kukosekana kwa taarifa za mapema za maendeleo ya miradi inayotekeleza katika maeneo mbalimbali nchini, hali ambayo ingesaidia kwa namna moja ama nyingine kunusuru miradi hiyo.

Ushauri umetolewa na Shirika la HHU linaloshughulika na ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya fedha za umma katika miradi ya afya na kuwataka wananchi kusaidia kufuatilia uwajibikaji wa viongozi wanaotekeleza miradi katika maeneo yao.

"Watu wengi wamekuwa wakiogopa kutoa taarifa za ubadhilifu wa miradi kwasababu ya kuhofia mambo mbali mbali lakini kwa hatua tuliofikia kwa sasa ni mambo ya utandawazi watu wasiogop"amsma Kelvin Mwinuka Mratibu wa HHU Njombe

Ufuatiliaji huo unapaswa kuzingatia kasi ya utekelezaji wa miradi, uwepo wa viashiria vya rushwa katika miradi inayotekelezwa pamoja na ubadhirifu wa fedha kwenye miradi.

"Wanaojihusisha na ubadhili watolewe taarifa kusudi sheria iweze kufuata mkondo wake vinginevyo tukiendelea kuwaacha bado itakuwa ni changamoto"amesema Akohek Mbapila Mkuu wa dawati la Kuzuia Rushwa Njombe.

Shirika la HHU linaendelea kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini, njombe ikiwa ni moja ya maeneo ambayo wakazi wake wamenufaika na elimu inayotolewa na ambao wanasema elimu hiyo ni msaada mkubwa katika kukabiliana na ubadhilifu katika miradi ya umma.
Hata hivyo viongozi wa serikali wanaaswa kudumisha uzalendo na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yao hususani pale wanapotekeleza Miradi ya umma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad