DIWANI WA KATA YA SANDALI AKABIDHI BAJAJI KWA VIKUNDI VYA WALEMAVU, WANAWAKE NA VIJANA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 19, 2023

DIWANI WA KATA YA SANDALI AKABIDHI BAJAJI KWA VIKUNDI VYA WALEMAVU, WANAWAKE NA VIJANA

Diwani wa kata ya Sandali iliyopo Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Christopher Mwansasu akikabidhi funguo kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha walemavu, Muhamad Musa Ndekezi katika kukamilisha mkopo wa asilimia 10 kutoka manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Mei 19, 2023.

DIWANI wa kata ya Sandali iliyopo Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Christopher Mwansasu leo Mei 19, 2023 amekabidhi bajaji sita kwa vikindi vya vijana, Wanawake na walemavu kupitia mkopo wa asilimia 10 unaotolewa na manispaa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi bajaji hizo amesema kuwa asilimia 10 hizo zinazotolewa kwa vijana ni makusanyo ya mapato ya ndani ya manispaa ya Temeke.

"Kazi hii sio ndogo ni kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani ambaye aliamua kusimamia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ili tuendelee kuitekeleza na tunaitekeleza kwa vitendo na vijana wanaona namna wanavyonufaika na rasilimali za Tanzania. 

"Mimi diwani wa kata hii ya Sandali natoa mikopo kwa vikundi sita ikiwa ni sehemu ya vikundi 32 ambavyo hadi leo vimenufaika na mikopo ya kata yetu. Amesema Mwansasu

Amesema kuwa Mikopo yote iliyotolewa kwa miaka miwili tangu amekuwa diwani hadi sasa inafikia zaidi ya milioni 380.


Mwansasu ametoa wito kwa Watanzania kuwa hizo ni fursa kwa wote kwaajili ya kusaidia kuinua maisha ya wananchi.

"Vijana wote amkeni leo mnaona bajaji zinakabidhiwa kwa vijana wenzenu msije mkakaa kwa kisikia maNeno hivi vitu vipo na vinafanyika hapa nchini."

Pia amewaomba wanaochukua mikopo hiyo kwenda kutekeleza na kusimamia vile inavyotakiwa na kutimiza malengo yake ili kila kikundi kijikwamue kiuchumi.

"Nilazima kuhakikisha fedha hiiinarejeshwa kwa taratibu zilizopangwa na inavyotakiwa ili iweze kusaidia watu wengine, nyinyi msiporejesha kwa wakati vikundi vingine vitakosa." Amesisitiza Mwanzasu

Akizungumzia kuhusiana na madereva wa bajaji hizo amesema kuwa wahakikishe wanawasimamia vizuri ili wawawezeshe kulipa mikopo hiyo ambapo watawezesha vikundi vingine kukopa.

Kwa upande wa katibu wa kikundi cha wanawake, Mwazani Lugoma amesema kuwa mkopo huo utawanufaisha katika kutimiza malengo yao.

Pia amewaomba vikundi vingine waende kuomba mkopo katika halmashauri zao kupitia kata zao kwani mikopo hiyo ipo na inakopeshwa.

Akizungumzia kuhusiana na jinsi watavyonufaika na Mkopo huo wa bajaji, Mwenyekiti wa Kikundi cha walemavu, Muhamad Musa Ndekezi amesema kuwa wamepokea mkopo wa asilimia 10kupitia halmashauri ya  Temeke kupitia kata ya Sandali... Nimshukuru Mh. Diwani kwa kuwa bega kwa bea na sisi tangu mwanzo mpaka sasa tunakabidhiwa bajaji, pia nimshukuru Rais Dkt.Samia kwa kutenga asilimia hizo ili ziweze kutunufaisha kiuchumi... Amesema

Kwa upande wa katibu wa kikundi cha wanawake, Mwazani Lugoma amesema kuwa mkopo huo utawanufaisha katika kutimiza malengo yao.

Pia amewaomba vikundi vingine waende kuomba mkopo katika halmashauri zao kupitia kata zao kwani mikopo hiyo ipo na inakopeshwa.

"Mje kata mtaelekezwa namna ya kuomba mikopo katiba zipo mtazisoma na kuzielewa mikopo ipo njoeni mtapata".
Matukio mbalimbali ya makabidhiano ya bajaji jijini Dar es Salaam leo Mei 19, 2023.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad