HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 6, 2023

Ziara ya Makamu wa Rais yaibua fursa lukuki

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Stergomena Tax akiteta jambo na baadhi ya mabalozi mara baada ya kikao  kumalizika jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Stergomena Tax akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris  aliyoifanya nchini hivi karibuni.
Mabalozi wa nchi mbalimbali  wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimaifa Stergomena Tax jijini Dar es Salaam.

*Rais Samia apongezwa kwa uongozi mahiri

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SERIKALI imesema kuwa ziara ya kikazi ya Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Devi Harris umetokana na ziara zilizofanywa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambazo zimekuja na mafanikio ya ujio wa Makamu wa Rais huyo.

Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tatu katika Bara la Afrika zilizotembelewa na Kiongozi huyu Mkuu wa Marekani tangu utawala wa Rais Joseph Biden kuingia madarakani, ni matokeo ya juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kukuza na kuimarsha diplomasia na ushirikiano wa kimataifa, na pia ni uthibitisho wa uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Marekani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Stergomena Tax amesema ishara ya ujio wa Makamu wa Rais wa Marekani kwa Tanzania inakwenda katika kujiimarisha katika mahusiano ya kidiplomasia kimataifa.

Amesema Makamu wa Rais wa Marekani alimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyofanya ya kuimarisha Demokrasia na kuboresha mazingia ya biashara na uwekezaji.

Tax amesema ziara ya Makamu wa Rais Kamala Harris imekuwa na mafanikio makubwa katika kuimarisha na kufungua maeneo mapya ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani.

Wakati wa ziara hiyo, Viongozi hawa Wakuu walifanya mazungumzo ya uwili, na Kamala na alitembelea Makumbusho ya Taifa na kuweka shada la maua kuwakumbuka wahanga wa shambulio la kigaidi la mwaka 1998 katika Ubalozi wa Marekani hapa nchini; na alifanya mazungumzo na vijana wajasiriliamali wa masuala ya ugunduzi wa teknolojia (startup association).

Katika ziara hiyo, Serikali ya Marekani ilitoa ahadi mbalimbali kwa Serikali ya Tanzania, na Mikataba na Hati za Makubaliano kadhaa ziliwekwa Saini

Katika makubaliano ni Serikali ya Marekani kujenga kiwanda kikubwa nchini Tanzania, ambacho kitakuwa cha pekee barani Afrika, cha kuchakata madini aina ya Nikel yanayotumika kutengenezea betri za gari za umeme kwa ajili ya soko la Marekani na duniani ifikapo mwaka 2026. Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa na Kampuni ya Life Zone Metals, na kampuni ya TechMet zinazomilikiwa kwa ubia na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Fedha la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (DFC). Kiwanda hiki kitatoa ajira kwa watanzania, na kuchangia katika pato la Taifa.

Amesema Mkataba mmoja na Hati mbili za makubaliano zilisainiwa ni Mkataba wa Msaada wa Maendeleo kati ya Tanzania na Serikali ya Marekani kupitia USAID wa kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.1 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi ulisainiwa na Mkataba wa Msaada wa Maendeleo kati ya Tanzania na Serikali ya Marekani kupitia USAID wa kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.1 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi ulisainiwa; na Waziri Tax amesema Hati ya Makubaliano kati ya Tanzania na Marekani ilisainiwa kupitia makubaliano hayo Serikali ya Marekani itatoa ushauri wa kitaalam na kujenga uwezo kwa wataalam kuhusu usimamizi wa bandari za Tanzania, hususan katika upanuzi wa bandari, vifaa vya kisasa na uendelezaji wa Bandari pamoja na Mkataba huo na Hati za Makubaliano hizo zilizosainiwa, Tanzania itanufauka kupitia ahadi za Serikali ya Marekani iliahidi kutoa nyongeza ya Dola za Marekani milioni 1.3 kupitia Shirika la Misaada la Marekani USAID kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya kuendelea kukabiliana na magonjwa ya mlipuko, Serikali ya Marekani kutoa zaidi ya Dola za Marekani bilioni 1.0 kwa ajili ya kuwawezesha wanawake wa Afrika walio katika sekta ya Umma, na sekta binafsi kushiriki shughuli za kiuchumi na kijamii, Serikali ya Marekani kuingia Makubaliano na Tanzania yatakayowezesha Marekani kuuza bidhaa za usafirishaji, uchukuzi, teknolojia ya digitali, na nishati safi zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 500, Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Msaada la Marekani USAID kutoa Dola za Marekani 600,000 kwa ajili ya kushirikiana na kampuni za mawasiliano na teknolojia ya sekta binafsi, na Serikali ili kupanua huduma za nishati safi na kutoa umeme kwa takriban vituo 100 vya afya katika maeneo ya magharibi, kati, na kusini mwa Tanzania. Mradi huo utawezesha kampuni za mawasiliano ya simu kuimarisha huduma za takwimu na kuwezesha vituo vya afya kutumia mifumo ya kidijitali katika utoaji wa huduma.

Hata hivyo amesema Serikali ya Marekani kuendelea kuwekeza katika Mpango wa Dharura wa Rais wa Kusaidia UKIMWI na Tanzania kuendelea kunufaika, ambapo Marekani inapanga kuwekeza Dola za Marekani milioni 433 katika kipindi cha miaka miwili ijayo ni Serikali ya Marekani kupitia Mpango wa Rais wa kupambana na Malaria na kutenga kiasi cha Dola za Marekani milioni 39 kwa mwaka 2024. Mradi huo unalenga kupambana na malaria, ikiwa ni pamoja na kusambaza vyandarua, dawa za malaria, vifaa vya uchunguzi wa haraka wa malaria, na dawa za kuzuia malaria kwa wajawazito, ambapo Tanzania itaendelea kunufaika, Mradi wa Miaka Mitano wa Heshimu Bahari wa Dola za Marekani milioni 8.4.

Aidha amesema mradi huo unakusudia kulinda mazingira ya bahari na kuongeza tija kwenye mfumo wa ikolojia ya bahari (ecological resilience and productivity of marines’ ecosystems), Kutenga Dola za Marekani milioni 16.4 katika Bajeti ya Marekani ya Mwaka 2024 kwa ajili ya kuendeleza demokrasia, haki, na programu za utawala nchini. Vilevile, kupitia USAID, Serikali ya Marekani inatarajia kutoa kiasi cha Dola za Marekani milioni 1 za ziada kwa ajili ya programu ambazo utekelezaji wake utaanza mwaka huu, Serikali ya Marekani kuipatia Tanzania kiasi cha Dola za Marekani milioni 1 kwa ajili ya miradi inayolenga kuondoa vikwazo vya uhuru wa kujieleza kwa umma na vyombo vya habari vya Tanzania, Serikali ya Marekani kutoa Dola za Marekani 400,000 kusaidia kazi ya Kituo cha Demokrasia kuleta pamoja wadau kujadili mageuzi zaidi ya kidemokrasia na sheria, na kuwajengea uwezo vijana kushiriki kwenye shughuli za kisiasa, Serikali ya Marekani kutoa Dola za Marekani milioni 16 kwa ajili ya mpango wa Kilimo Tija.

Amesema Mpango huo unalenga kusaidia wakulima nchini, hususan wanawake na vijana katika kukabiliana na changamoto za usalama wa chakula na Tanzania na Marekani kuanzisha majadiliano ya kuongeza muda wa ukomo wa visa (Visa ya miaka mitano).

Ziara ya Kamala Harris, Makamu wa Rais wa Marekani nchini, imekuwa na mafanikio makubwa katika kuimarisha na kufungua maeneo mapya ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani, na kuitangaza nchi yetu duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad