HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 20, 2023

WAZIRI JAFO AUPONGEZA MKOA WA PWANI KWA KAMPENI YA UPANDAJI MITI

 

Mtambo wa Gas uliotolewa na Kampuni ya Taifa Gas  katika Shule ya ya Sekondari ya Wasichana Ruvu iliyopo Mkoani Pwani.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo akizungumza  jana Aprili 19, 2023 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu iliyopo Mlandizi Wilayani Kibaha mkoani Pwani wakati wa kuzindua Kampeni ya utunzaji mazingira na matumizi ya nishati mbadala kwa Mkoa huo iliyoandaliwa na Benki ya NMB,  Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Mkoa wa Pwani, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Taifa Gas.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon  akitoa salamu za Mkoa ambapo alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge bubakari 

Waziri Jafo akizindua mtambo huo wa Taifa Gas  jana Aprili 19, 2023 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu iliyopo Mlandizi Wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Mwakilishi wa Kampuni ya Taifa Gas Angella Bhoke akizungumza  jana Aprili 19, 2023 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu iliyopo Mlandizi Wilayani Kibaha mkoani Pwani wakati wa kuzindua Kampeni ya utunzaji mazingira na matumizi ya nishati mbadala kwa Mkoa huo iliyoandaliwa na Benki ya NMB,  Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Mkoa wa Pwani, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Taifa Gas.


Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo ameupongeza Mkoa wa Pwani kwa kuweka kampeni ya upandaji miti ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Jafo ameyasema hayo jana Aprili 19, 2023 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu iliyopo Mlandizi Wilayani Kibaha wakati akizundua Kampeni ya utunzaji mazingira na matumizi ya nishati mbadala kwa Mkoa huo iliyoandaliwa na Benki ya NMB Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Mkoa wa Pwani, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Taifa Gas.

Waziri Jafo amesema kuwa kampeni hiyo itasaidia kutunza mazingira pia utasaidia kutangaza teknolojia mbadala ya matumizi ya nishati mbadala baada ya kupunguza matumizi ya miti kama nishati kwa ajili ya kupikia na matumizi mengine ya binadamu ya kila siku.

Amesema kuwa Mkoa wa Pwani ni moja ya mikoa minne ambayo imeathirika kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa mazingira nchini lakini baada ya kupata maelekezo kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutaka Mikoa hiyo iweke mipango ya kukabiliana na hali hiyo Mkoa umejiongeza kwa kuwa na kampeni hizo za kukabiliana na changamoto za mazingira.

Waziri Japo amezindua mtambo mkubwa Gas shuleni hapo Aprili 19 ambao utakua ukitumika kwenye jiko la shule ikiwa ni katika kuhakikisha wameachana na matumizi ya kuni na mkaa .

Awali akimkaribisha Waziri Jafo akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John amesema kuwa Mkoa umeweka mikakati mbalimbali ili kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti million 13.5 lakini hadi sasa tayari Mkoa umeshapanda miti milioni 9.7 ikiwa ni zaidi ya asilimia 85 ya malengo ili waliyojiwekea ili kurejesha uoto wa asili uliokuwepo awali kabla ya uharibifu wa mazingira.

Amesemakuwa Mkoa wa Pwani umejipanga kuwaondoa vijana ambao wamejiajiri kwenye biashara ya ukataji wa miti na kuchoma mkaa kwa kuwakusanya na kuwapa ajira mbadala.kwenye Viwanda vitakavyo anzishwa vya nishati mbadala.

Mwakilishi wa Kampuni ya Taifa Gas kurugenzi Anjela Bhoke amesema kuwa kila mwaka hekari 400,000 za miti zinapotea kutokana na matumizi mbalimbali ya miti ambapo moja ya mikakati yao waliyojiwekea ni kujenga Kiwanda cha kutengeneza mitungi ya nishati mbadala (Gas) ambapo wako tayari kusambaza gesi hiyo majumbani na kwenye taasisi za umma.

Pia wameandaa Tuzo kwa Waandishi wa Habari itakayotolea baada ya wanahabari hao kushindanishwa kutokana na umahiri wao wa kuandika makala kwenye magazeti ,Radio na Luninga.

Mwakilishi wa benki ya NMB Seka Urio amesema kuwa wametenga kiasi cha shilingi milioni 470 kwa ajili ya shule zitakazopanda miti 2,000 na kuitunza kwa asilimia 80 ambapo itapatiwa milioni 50, huku mshindi wa pili kwa kupanda miti 1,500 akipata Milioni 30 akiitunza kwa asilimia 70 na watatu atapata milioni 20 kwa kupanda miti 1,000 itakayokuwa imetunzwa kwa asilimia 70.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad