HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 15, 2023

WAANDISHI WATATU WAPATA ULAJI UWT KIBAHA

 

Mwandishi wa Chanelten na Radio Magic FM Margaret  Malisa akipokea barua ya uteuzi kutoka kwa Katibu wa UWT Kibaha Mjini Mariam  Mgasha.

Baadhi ya Viongozi wa UWT Wilaya ya Kibaha  wakiwa  kwenye Ofisi ya UWT Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.

Na Khadija  Kalili, PWANI
UMOJA  wa Wanawake Wilaya ya Kibaha Mjini (UWT) wamefanya uteuzi kwa Waandishi wa Habari watatu kutoka Chanel ten  na Magic Fm Radio,  Margaret Malisa, Diwani wa Viti Maalumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Selina Wilson  na  Mwandishi   wa Magazeti ya Uhuru pamoja na Redio Uhuru  Mwamvua Mwinyi   kuwa Wajumbe wa Kamati ya Habari na Mawasiliano ya UWT Wilaya ya Kibaha Mjini .

Uteuzi huo  una lengo kupanua wigo wa utoaji habari za Chama Cha Mapinduzi  (CCM) hususani kutangaza kazi zinazofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni katika kutekeleza ilani ya CCM ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya ya kibaha  Mkoani Pwani.

Mwenyekiti wa UWT  Wilaya ya Kibaha Elina Mgonja amesema baada ya kuwakabidhi barua zao za  uteuzi huo Wajumbe hao amesema kuwa  kuteuliwa kwao kumefanywa  Baraza maalumu  la dharula la Wajumbe wa UWT Wilaya ya Kibaha.

Mwenyeki huyo amewataka Waandishi hao wa habari kutumia  kalamu zao  katika kuhabarisha umma mazuri yanayofanywa na CCM   katika utekelezaji wa ilani.

 " Kamati tendaji tumemua kuwateua hawa Waandishi , ili kuleta nguvu ya pamoja katika kutangaza kazi zinazofanywa na serikali na tunaamin kuwa , watafanya vizuri kwani ni watumishi wa vyombo vinavyomilikiwa na Chama Chetu cha Mapinduzi  (CCM) hivyo  itakuwa ni rahisi kwao kutangaza kazi zilizofanywa katka utekelezaji wa Ilani ", amesema Mwenyekiti huyo.
Aisha 
Baraza hilo pia limepokea taarifa za kazi za Madiwani  wa  Viti Maalumu, pamoja na  kuweka mipango na  mikakati  ya ushindi wa kishindo  mwaka 2024/25.
 
Mgonja ametumia   fursa hiyo   kuwataka madiwani  kufuata kanuni za baraza la UWT  ikiwa ni pamoja na kupeleka taarifa zao za kazi  kila  baada ya miezi mitatu,  kuheshimiana pamoja na   kuhudhuria vikao pia  kutoa taarifa pindi wanapopata dharula.

Mbali ya Kamati ya Habari na Mawasilano pia  Baraza hilo  limeunda Kamati zingine  ikiwemo  ya   Kamati ya Uchumi na Fedha ,  Kamati ya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wanawake  na Makundi Maalum, 

Kamati ya Maendeleo , Kamati ya Afya na  Kamati ya Hamasa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad